banner58

Sheria yaja kupima ukimwi kutumia mate

Waziri Ummy alisema kipimo cha sasa cha ukimwi ni kupitia damu

Sheria yaja kupima ukimwi kutumia mate

Waziri Ummy alisema kipimo cha sasa cha ukimwi ni kupitia damu

31 May 2018 Thursday 15:42
Sheria yaja kupima ukimwi kutumia mate

Na Mwandishi Wetu

SHERIA mpya inatarajiwa kutungwa kuwafanya watanzania waweze kupima ugonjwa wa ukimwi kwa kutumia mate, badala ya damu kama ilivyozoeleka, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameliambia Bunge.

Alikuwa akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliotaka kujua mikakati ya serikali katika kuhakikisha kiwango cha maambukizi ya ukimwi kinapungua na njia za kuwafanya watu wengi wapime afya zao.

Waziri Ummy alisema kipimo cha sasa cha ukimwi ni kupitia damu, na endapo kama tutalazimika kutumia mate basi kuna mabadiliko ya sheria yanatakiwa.

Alisema kuwa serikali tayari imekwisha andika kwa wahusika kuhusu mabadiliko ya sheria hiyo itakayomwezeshe mtu kujipima mwenyewe virusi vya ukimwi kwa kutumia mate.

Aliongeza kuwa endapo mtu huyo atakuwa amebainika kuwa na virusi vya ukimwi, basi atakwenda kwenye kituo cha afya kwa ajili ya kupatiwa dawa za kufubaza bure.

Alisema dawa hizo zipo na kuwataka wote waliobanika kuwa na virusi kutokuwa na wasiwasi kwani wataingizwa kwenye mpango wa dawa za kufubaza na maisha yao yatakuwa safi na salama.

Wataalam wanasema anachotakiwa mtu kufanya ni kuchukuwa ute au mate yaliyopo katika kinywa chake kwa kutumia vifaa maalumu na kusugua katika fizi za juu na chini kisha kuweka ute huo katika kipimo ambapo baada ya dakika kati 20 na 40 jawabu hupatikana

Lakini ufanisi wake ni kwa asilimia 92 wakati asilimia 8 inayobakia ndipo anaweza kupatikana mtu mmoja kuwa na majibu chanya wakati majibu yake ni hasi.

Uwezo wa kifaa hicho unawekwa wazi kuwa unaweza kutambua aina mbili za virusi vya UKIMWI yaani HIV namba 1na HIV namba 2 ambavyo hapo awali ilikuwa vigumu kuweza kutambua kwa kipimo kimoja.

Inakadiriwa kuwa bei ya kifaa hicho kinachotengenezwa na kampuni ya Ora Sure Technologies ya nchini Marekani inaweza kuwa zaidi ya shilingi 34,000.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.