Shuhuda atoa ushuhuda jinsi msaidizi wa Membe alivyotekwa

Shuhuda atoa ushuhuda jinsi msaidizi wa Membe alivyotekwa

08 July 2019 Monday 15:47
Shuhuda atoa ushuhuda jinsi msaidizi wa Membe alivyotekwa

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
TAKRIBANI watu saba wakiwa na bastola wanadaiwa kumteka Allan Kiluvya ambaye ni msaidizi wa waziri wa zamani, Benerd Membe. Tukio la kutekwa Allan limetokea Julai 6, 2019 majira ya usiku huko Mbezi Beach jijni Dar es Salaam.

Shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Magreth amesema kabla ya kutekwa, alikuwa na Allan na mwezake Agness katika hotel ya Juliana iliyopo eneo la Afrikana, wakipata vinywaji.

''Baada ya kutoka baa,  Allan aliturejesha nyumbani  hapa Jongoo nikafungua geti akaingia na gari lake  ili amsalimie mama na kweli alimsalimia kwa kuwa alikuwa ajalala. 

''Baada ya hapo akarudisha gari nyuma ili atoke na ndipo nikamuomba fedha akaniambia njoo nje ya geti,'' amesema na kuongeza

''Baada ya muda wakati Allan akiweka gari yake vizuri nikaona gari aina ya Landcruser linakuja mara watu saba wakawa wamezunguka gari la Allan na mmoja akatoa bastola na  wengine wakaanza  kumpiga,

''Allan akaniambia kimbia, mmoja wa wale watekaji akasema mkamate na huyo dada ndio nikaingia ndani huku nikipiga kelele za kuomba msaada,
''Cha ajabu walimchukua Allan na simu moja na waliacha kila kitu katika gari''.

Magreth amesema mara baada ya kutokea tukio hilo baadhi ya watu waliofika hapo wakiwamo madereva bodaboda walidai  kabla ya tukio gari hilo lilipita kwa zaidi ya mara tatu mtaani hapo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kinondoni,  Mussa Taibu amesema ndugu wa Allan ameripoti tukio hilo Polisi na kwamba wanalifuatilia. " Tunaendelea kulifuatilia  kujua ni kwa namna gani alichukuliwa lakini siwezi kusema ametekwa kwa sababu bado hatujathibitisha,'' alisema kamanda huyo jana Julai 7, 2019

PICHANI JUU; Ni Allan Kiluvya

Updated: 08.07.2019 16:48
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.