Sita wafariki, 22 wajeruhiwa katika ajali

Sita wafariki, 22 wajeruhiwa katika ajali

22 July 2019 Monday 12:28
Sita wafariki, 22 wajeruhiwa katika ajali

Na mwandishi wetu, Kahama
TAKRIBANI watu sita wamefariki dunia na wengine 22 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea  eneo la nyambula kata ya Ngogwa Wilayani  Kahama mkoani Shinyanga

Ajali hiyo imetokea usiku Julai 21, 2019 baada ya gari aina ya Land cruiser  yenye namba za usajili T 477 ATC kugongana na Toyota  hiace yenye namba za usajili T 710 AZZ.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard Abwao amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa hiace iliyokuwa na abiria ikitokea Kakola kwenda Kahama mjini.

"Hadi sasa watu wanne wamefariki na wengine 12 wamejeruhiwa na wapo katika hospitali ya Kahama. Ukweli ni kuwa barabara ya Kakola hadi  Kahama inavumbi jingi na magari yanayopita ni mengi hii ni kutokana na ongezeko la watu katika machimbo mapya ya Kakola namba 9,'' amesema

Amesema ili kudhibiti ajali kutakuwepo na operesheni maalum katika barabara hiyo ikiwamo kuondoa magari mabovu

Kamanda huyo amesema baadae anatarajia kutoa taarifa rasmi  za ajali na majina ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.

Updated: 22.07.2019 14:58
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.