Spika Ndugai azuia wakurugenzi wa Uchaguzi kuguswa

Spika Ndugai azuia wakurugenzi wa Uchaguzi kuguswa

13 September 2018 Thursday 11:18
Spika Ndugai azuia wakurugenzi wa Uchaguzi kuguswa

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amemzuia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Susan Kolimba kujibu maswali ya Mbunge wa Kitambile Masoud Abdallah Salim ambapo mojawapo lilihoji kuwa, lini serikali itapeleka mswada bungeni wa kubadili sheria inayoruhusu Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Salim aliuliza amswali hayo leo tarehe 13 Septemba 2018 bungeni jijini Dodoma, ambapo amedai kuwa, kitendo cha wakurugenzi wa halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi, kinaminya uhuru wa demokrasia kutokana kwamba wakurugenzi hao ni makada wa chama tawala nchini CCM na hivyo ikifika kipindi cha uchaguzi wanakuwa marefa wa kuisaidia CCM kupata ushindi.

Mbunge huyo alilielekeza maswali mawili ya nyongeza katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambapo swali lilingine aliihoji wizara hiyo kwamba, kwa nini serikali imeshindwa kudhibiti mfumuko wa bei ya sukari kitendo kinachochangia ugumu wa maisha kwa wananchi.

Baada ya Salim kuuliza maswali hayo, Spika Ndugai aliyakataa maswali hayo akisema kuwa hayaendani na swali lake la msingi pamoja na kuuliza katika wizara isiyo sahihi, lakini pia kuhusu swali lake mfumuko wa bei ya sukari, alisema litajibiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.