banner68
banner58

Tanzania yaja na sera mahususi kwa diaspora, sasa kuchangia uchumi

Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbali mbali zinazowawezesha diaspora kuchangia maendeleo ya uchumi

Tanzania yaja na sera mahususi kwa diaspora, sasa kuchangia uchumi

Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbali mbali zinazowawezesha diaspora kuchangia maendeleo ya uchumi

17 April 2018 Tuesday 11:55
Tanzania yaja na sera mahususi kwa diaspora, sasa kuchangia uchumi

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kuwa itaandaa sera mahususi kuhusu Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi (diaspora) ili waweze kuchangia maendeleo ya nchi ikiwemo viwanda.

Hayo yamelezwa Bungeni leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, William Ole Nasha, kwa niaba ya Waziri wa mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga, wakati akjibu swali la nyongeza la Mbunge wa viti Maalum Hadija Nassiri.

Mbunge huyo alitaka kujua idadi ya watanzania waliokuwa wanaishi nje ya nchi na ambao wameajiriwa hapa nchini na mchangao wao katika uchumi wa viwanda.

Akijbu swali hilo, Naibu Waziri Ole Nasha, alisema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada mbali mbali zinazowawezesha diaspora kuchangia maendeleo ya uchumi.

Akitolea mfano alisema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita (2013-2017) diaspora wa Kitanzania walituma nyumbani zaidi ya dola 2,284 milioni ambazo zimetumika kuendeleza uchumi wa nchi.

Kiasi hicho cha fedha kilitumika kununua nyumba 108 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na pia uwekezaji mwingine, alifafanua.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo alisema kuwa ili kuwafanya diaspora hao kuchangia uchumi wa nchi ipasavyo serikali itaandaa sera mahususi kwa ajili hiyo.

“Tutatakuja na sera mahususi ya diaspora ambayo itawawezesha kuchangia vizuri uchumi wa Tanzania hasa katika ujenzi wa viwanda,” alieleza.

Akizungumza hivi karibuni mmoja wa diaspora, Dk Mselly Mbwambo alikaririwa akisema kuwa Watanzania wanaoishi nje wanaweza kuwa chanzo muhimu na kutoa usaidizi wa utafiti na ufumbuzi wa masuala mbali mbali.

Japan, Jamhuri ya Korea na Taiwan, China ni mifano ya uchumi ambayo ulitegemea wanadiaspora wao kama vyanzo vya ujuzi.

Serikali katika nchi hizi, ili kuinua uchumi wao, ziliwahimiza wanafunzi wenye elimu ya kigeni kurudi nymbani au hata kuanzisha mitandao ya kubadilishana maarifa kati ya Serikali na wanadiaspora anasema.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.