Treni abiria yapata ajali, 32 wajeruhiwa

Treni abiria yapata ajali, 32 wajeruhiwa

18 June 2019 Tuesday 09:54
Treni abiria yapata ajali, 32 wajeruhiwa

Na mwandishi wetu, Dodoma
TRENI ya abiria imepata ajali, mabehewa mawili ya daraja la tatu yameanguka na takribani watu 32 wamejeruhiwa.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 5:30 usiku Juni 17, 2019  jijini Dodoma, imehusisha lori na treni ya abiria iliyokuwa ikielekea Dar es Salaam kutoka mikoa ya Mwanza na Kigoma.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha  tukio hilo na kwamba jeshi la polisi limeweka ulinzi wa kutosha kudhibiti mali  na mizigo ya abiria.

Kamanda Muroto amesema polisi wanamsaka dereva wa lori ambaye inadaiwa amekimbia baada ya kuruka kutoka garini.

Amesema kwa sasa shughuli ya kuondoa mabehewa yaliyoanguka  inaendelea.

Updated: 19.06.2019 09:42
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.