Tundu Lissu :Nitarejea Tanzania baada ya Oktoba 8

Tundu Lissu :Nitarejea Tanzania baada ya Oktoba 8

10 September 2019 Tuesday 06:21
Tundu Lissu :Nitarejea Tanzania baada ya Oktoba 8

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MWANASIASA, Tundu Lissu amesema baada ya Oktoba 8, 2019 atatangaza rasmi tarehe ya kurudi nyumbani Tanzania

Hatua hiyo inafuatia baada ya kuahirisha tarehe ya Septemba 7, 2019 kurudi Tanzania. Tarehe hiyo ya Septemba 7 ilikuwa ni miaka miwili tangu ashambuliwe kwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma.

Akizungumza na Azaniapost kwa njia ya simu, Lissu amesema hatma ya kurudi nyumbani itafuatia mara baada ya kukutana na madaktari wake Oktoba mosi na kisha Oktoba 8, 2019.

‘‘Oktoba Mosi nitakutana na madaktari wangu kwa ajili ya kupata viatu vya kuvaa na kisha Oktoba 8, 2019 ndio nitajua hatma yangu. Baada ya hapo ndio nitapanga tarehe ya kurejea nyumbani Tanzania,’’ amesema Lissu

Lissu anasema bado anasubiri kupata ridhaa ya madaktari wake iwapo anaweza kurudi nyumbani.

''Nilishasema kwamba ninasubiri nipate uamuzi wa mwisho wa madaktari wangu, nasubiri waniambie sasa unaweza kwenda nyumbani. Wakiniambia hivyo nitaanza kupanga mipango ya safari ya nyumbani.

Alipoulizwa juu ya ikiwa bado ana nia ya kugombea urais amesema, iwapo chama chake pamoja na vyama rafiki vitampa wito wa kuviwakilisha katika kinyanganyiro cha urais mwakani, atagombea na kuongeza kuwa bado hajabadilisha msimamo wake hata kidogo.

''Katiba ya Tanzania inasema uwe umepatikana na hatia ya kosa kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma. Hatia ni kwamba umeshtakiwa, ukajitetea, utetezi wako haukutosha ukapatikana na makosa ndio katiba ya Tanzania itakuwa inakuzuwia'' alifafanua Lissu.

Tundu Lissu amekuwa nchini Ubelgiji akipokea matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mchana wa Septemba 7 mwaka 2017 mjini Dodoma alipokuwa akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.