Uhakiki mwingine wa miezi miwili waja, safari hii ni wa mawasiliano asema naibu Waziri

Uhakiki mwingine wa miezi miwili waja, safari hii ni wa mawasiliano asema naibu Waziri

01 June 2018 Friday 12:11
Uhakiki mwingine wa miezi miwili waja, safari hii ni wa mawasiliano asema naibu Waziri

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashata Nditiye, amesema kuwa atafanya ziara ya miezi miwili kukagua na kuhakikisha kuwa maeneo mengi yasiyo na mawasiliano yanapata huduma hiyo.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Hadija Hassan Abood (CCM) aliyemtaka Naibu Waziri huyo kutembelea kata za Mapanda, Ikwera, Tazara na Ihano mkoani Iringa ambako wananchi wamejengewa minara lakini hakuna mawasiliano.

Mbunge huyo alisema kuwa wananchi wa kata hizo wanapata shida sana za mawasiliano bila sababu yoyote.

Akijibu, Naibu Waziri Nditiye, alisema atafanya ziara kwa kushirikiana na maafisa wa mfuko wa mawasiliano kwa wote na kuangalia maeneo yenye changamoto na kuziweka kwenye bajeti.

Alibainisha kuwa kuna baadhi ya maeneo yana minara lakini hayana mawasilian kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ukosefu wa umeme na kijiografia.

Aliuagiza mfuko wa mawasiliano kwa wote Tanzania kuyafanyia kazi maeneo yenye changamoto za aina hiyo.

Akijibu swali lingine kuhusiana na barabara, Naibu Waziri huyo alisema kuwa kazi ya kuunganisha miundombinu ya vijijni ni wakala wa barabara vijijni (Tarura).

Swali hilo liliulizwa na Mbunge wa Kwela Ignas Malocha(CCM) aliyetaka kujua mpango wa kiuchumi wa serikali kutengeneza barabara za vijijini kuunganisha na za mikoa.

Naibu waziri huyo alisema kuwa ujenzi wa barabara za vijijini unafanywa na Tarura wao wizara wanafanya mchakato tu. Alisema kuwa mapendekezo yanatoka kuanzia baraza la madiwani ambao wanapeleka kwenye kamati ya ushauri ya mkoa (RCC).

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Majenge 2018-06-01 12:40:30

Itapendeza