Uhakiki taasisi za kidini, jamii  awamu ya pili waanza

Uhakiki taasisi za kidini, jamii  awamu ya pili waanza

18 June 2019 Tuesday 10:51
Uhakiki taasisi za kidini, jamii  awamu ya pili waanza


Na mwandishi wetu, Dodoma
SERIKALI imesema zoezi la uhakiki wa taarifa za jumuiya za kijamii na kidini  nchi nzima awamu ya pili unaanza.

Taarifa ya ofisi ya  msajili wa jumuiya za kijamii na kidini,wizara ya mambo ya ndani ya nchi inasema awamu ya pili ya zoezi hilo itaanza Juni 23 hadi Julai 2, 2019.

Zoezi hilo litafanyika jijini Dodoma na litahusisha taasisi/jumuiya zilizopo katika mikoa ya Morogoro,  Dodoma, Singida na Manyara.

"Zoezi la uhakiki awamu ya pili litafanyika katika ofisi ya zamani ya kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni'' inaeleza taarifa hiyo ya Juni 15, 2019.
Katika uhakiki huo nyaraka zifuatazo zinahitajika;
Cheti halisi cha usajili na kivuli cha cheti hicho, Stakabadhi ya mwisho ya malipo ya ada iliyolipwa na Katiba ya Jumuiya/taasisi iliyopitishwa na msajili

Updated: 18.06.2019 10:57
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.