Ujenzi mradi wa umeme Rufiji waanza

"Kazi anazoanza nazo leo ni upasuaji wa miamba ili kuruhusu maji kupita  kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme".

Ujenzi mradi wa umeme Rufiji waanza

"Kazi anazoanza nazo leo ni upasuaji wa miamba ili kuruhusu maji kupita  kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme".

15 June 2019 Saturday 09:56
Ujenzi mradi wa umeme Rufiji waanza

Na mwandishi wetu, Rufiji
MKANDARASI wa mradi wa umeme wa Rufiji, kampuni ya JV Arab Contractors na Elsewedy Electric leo Juni 15, 2019 anaanza rasmi kazi za ujenzi wa mradi huo.

Hayo yamesemwa Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani Juni 14, 2019 mara baada ya kukagua kazi za maandalizi ya awali ya ujenzi wa mradi huo akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na watendaji wengine kutoka kampuni ya mkandarasi, Wizara ya Nishati na  TANESCO.

Mkandarasi  anaanza ujenzi ikiwa ni baada ya kufanya matayarisho mbalimbali  ikiwemo upelekaji wa vifaa vitakavyotumika ktk shughuli za ujenzi, uwepo wa kambi za wafanyakazi, Ofisi na kukamilisha kazi nyingine za awali ambapo kwa mujibu wa mkataba.   Alipewa miezi sita ya kufanya kazi hizo ambayo ukomo wake ulikuwa Juni 14, 2019.

Dkt Kalemani amesema kazi anazoanza nazo leo ni upasuaji wa miamba ili kuruhusu maji kupita  kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme.

Amesema kazi nyingine za awali zitakazofanywa ni kujenga daraja la muda litakaloruhusu upitishaji wa vifaa kwenda kwenye eneo jingine la kazi pamoja na ujenzi wa daraja la kudumu.

Dkt Kalemani ameeleza  Mkandarasi ameahidi kukamilisha mradi huo ifikapo mwezi Juni, mwaka 2022 na mradi utatekelezwa kwa kasi na ikiwezekana, megawati zote 2115 zitapatikana kwa wakati mmoja.

Kuhusu vifaa vitakavyotumika kwenye mradi huo, Dkt Kalemani aliwataka kutumia vifaa vinavyopatikana nchini na kwa vifaa visivyopatikana nchini, vitanunuliwa baada ya kupata kibali maalum.

Pia aliagiza Wataalam wa ndani kupewa kipaumbele katika ujenzi wa mradi huo, ili waweze kusimamia mradi huo mara baada ya mkandarasi kukamilisha kazi.

Aidha, aliwapongeza TANESCO na TANROADS kwa kusimamia mradi huo ipasavyo, na kuwaagiza kuendelea kuwasimamia wakandarasi usiku na mchana

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.