UPDATES: Mama Maria Nyerere arejeshwa nchini kwa ndege, kuendelea na matibabu

UPDATES: Mama Maria Nyerere arejeshwa nchini kwa ndege, kuendelea na matibabu

05 June 2019 Wednesday 17:49
UPDATES: Mama Maria Nyerere arejeshwa nchini kwa ndege, kuendelea na matibabu

MKE wa rais wa zamani wa Tanzania Maria Nyerere amesindikizwa leo Juni 5, 2019 na maafisa wa Uganda ambako atapanda ndege kurejea nyumbani baada ya kuugulia nchini Uganda.

Anaondoka kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe kwa ndege rasmi aliyopewa na rais wa Uganda Yoweri Museveni hadi mjini Dar es salaam ambako anatarajiwa kuendelea na matibabu zaidi.

Rais Museveni ameripotiwa kutohudhuria sherehe za siku ya mashahidi wa Uganda katika eneo la Namugongo kwa ajili ya kumtembelea Mama Maria mjini Kampala

katika hospitali mjini Kampala.

Duru zinasema kuwa ilibidi rais Museveni kumtuma wawakilishi kwenye tukio la siku ya mashahidi wa Uganda ili kuwaepusha waumini kusubiri kwa muda mrefu , ili aweze kwenda kumuona Mama Maria Nyerere ambaye alikuwa katika hospitali moja mjini Kampala.

 Museveni alisema kuwa hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kuwa na mchango mkubwa kwa kipindi cha miaka milioni nne kwa Afrika zaidi ya Mwalimu Julius.

Duru zinasema kuwa Mama Nyerere mwenye umri wa miaka 88, alipata matatizo ya kiafya usiku kabla ya tukio la kumkumbuka mumewe Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Tangu mwaka 2009, waumini wa kanisa katoliki wamekuwa wakifanya ibada katika hekalu la Namugongo kwa ajili ya kumkumbuka mwalimu Nyerere.

Mama Maria Nyerere ambaye ni mke wa rais wa zamani wa Tanzania alikuwa nchini Uganda kwa ajili ya ibada maalum ya kukumbuka mchango wa hayati Mwalimu juliasi Nyerere kwa Afrika na Ukristo.

Juni Mosi, rais Yoweri Museveni wa Uganda na Mama Maria Nyerere walishiriki pamoja ibada hiyo maalumu iliyofanyika katika hekali la mashahidi wa Uganda la Namugongo.

Nyerere alitoa mchango wa zana kuwasaidia waasi wa Bwana Museveni kwa ajili ya kuung'oa madarakani utawala wa rais Idi Amin.

Bibi amekuwa akisafiri kwenda hadi Namugongo Uganda kwa miaka 13 mfulurizo kwa ajili ya sherehe za kuwakumbuka mashahidi wa Uganda.

BBC

Updated: 06.06.2019 07:56
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.