UPDATES:Viongozi watano ACT Wazalendo waliokamatwa, waachiwa

UPDATES:Viongozi watano ACT Wazalendo waliokamatwa, waachiwa

14 September 2019 Saturday 14:35
UPDATES:Viongozi watano ACT Wazalendo waliokamatwa, waachiwa

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

JESHI la polisi  jioni ya leo Septemba 9, 2019 limewaachia kwa  dhamana  viongozi watano wa chama cha ACT wazalendo. Viongozi hao  walikuwa wanashikiliwa  katika  kituo cha Polisi Chang'ombe  Temeke jijini Dar es Salaam kwa mahojiano.

Waliokamatwa ni Katibu wa Itikadi, uenezi na Mawasiliano Kwa Umma Taifa, wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu, Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Soud Salum, Katibu wa Uchaguzi Mkoa , Risasi Semasaba na Katibu wa Ngome ya Vijana wa Kata ya Azimio, Said wamekamatwa na askari wa Jeshi la Polisi wakiwa katika Shughuli ya Ufunguaji wa Matawi Mapya ya Chama hicho leo Septemba 9,2019, Katika Jimbo la Temeke, Kata ya Azimio jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti kamati ya itikadi, uenezi na mawasiliano kwa umma wa chama hicho, Salim Biman amesema Polisi waliwashikilia viongozi hao kwa tuhuma za  kukosa kibali cha ufunguaji wa matawi.


 

Updated: 14.09.2019 23:01
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.