Viboko, Mamba sasa kuuzwa

Viboko, Mamba sasa kuuzwa

19 August 2019 Monday 06:02
Viboko, Mamba sasa kuuzwa

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Khamis Kigwangala amesema Serikali itaanza kuuza asilimia 10 ya mamba nje ya nchi kutokana na ongezeko kubwa la wanyama wakali kuingia kwenye makazi ya watu.

Vilevile Serikali itauza viboko wote waliopo kwenye maeneo yenye maji kama maziwa, mabwawa na mito iliyopo mjini.

Waziri amesema Serikali imejhitahidi vya kutosha kuhakikisha suala la ujangiri linaisha nchini na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa bali changamoto iliyopo, ni wanyama hao kuingia kwenye makazi ya watu.

“Uhifadhi na ulinzi wa maliasili nchini umeimarika na tumepata mafanikio makubwa sana. Ujangili tumeudhibiti kwa mafanikio makubwa sana’’ amesema waziri huyo na kuongeza “Changamoto mpya imezaliwa, wanyama wakali na waharibifu wamezidi na wanavamia maeneo ya watu, tumeamua kuuza asilimia 10 ya mamba wote nchini”

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.