Vigogo Rahco waendelea kusota rumande, mmoja alazwa

Vigogo Rahco waendelea kusota rumande, mmoja alazwa

17 June 2019 Monday 14:20
Vigogo Rahco waendelea kusota rumande, mmoja alazwa

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea na ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa Kampuni Hodhi ya Mali za Shirika la Reli (RAHCO) baada ya mshtakiwa wa pili mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH)

Wakili wa Takukuru, Maghela Ndimbo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini mshtakiwa wa pili anaumwa na amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

"Shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi tunaye hapa lakini mshtakiwabwa pili anaumwa hivyo naiomba mahakama hii ipangebtarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa,"alidai Ndimbo

Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka  siku ya shauri hilo linapokuja mahakamani hapo waje na shahidi mwingine ili aweze kutoa ushahidi pindi shahidi wa kwanza atakapomalizia kutoa ushahidi wake.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 24 na Juni 25,2019 itakapokuja kwa ajili ya ushahidi.

Mbali na Mwinyijuma washtakiwa wengine ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Rahco, Benhardard Tito; Mwanasheria wa zamani wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe

Katika kesi hiyo tayari shahidi mmoja kwa upande wa mashtaka Regnald Malele ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa Shirika la Reli Tanzania(TRC),ametoa ushahidi na bado hajamaliza kutoa ushahidi wake.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manane ikiwamo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kuisababishia Rahco hasara ya dola za Marekani 527,540,000.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.