Vigogo tisa NSSF wapandishwa kortini kwa uhujumu uchumi

Vigogo tisa NSSF wapandishwa kortini kwa uhujumu uchumi

01 October 2019 Tuesday 16:51
Vigogo tisa NSSF wapandishwa kortini kwa uhujumu uchumi

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

WAFANYAKAZI tisa kutoka makao makuu Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSf) wamefikishwa Katika mahahama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la utakatishaji fedha zaidi ya bilioni 2

Watuhumiwa hao ni Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Jamila Vulu, Mhasibu, Dominic Mbwete, Mhandishi wa Hundi, Abdulrahaman Njozi, Mhasibu Mwandamizi, James Oigo, Mhasibu Mkuu, Hellen Peter, Mhasibu kitengo cha Madeni, Invonne Kimaro, Mhasibu dawati la Uchunguzi, Restiana Lukwaro, Kaimu Rasilimaliwatu, Tikyeba Alphonce na Meneja Uhakiki, Amiri Kapera,

Leo Oktoba 1, 2019 akisoma hati ya mashtaka hayo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa shtaka wanaokabiliwa washtakiwa hao ni la uhujumu uchumi.

Simon amedai kati ya Julai Mosi, 2016 na Septemba 4, 2017 maeneo ya Dar es Salaam washtakiwa hao pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani walikula njama na kutakayisha fedha kiasi cha zaidi ya bilioni 2 wakionyesha hundi hizo halali zimetolewa na bodi ya wadhamini ya NSSF huku wakijua si kweli.

Katika shtaka la pili kati ya Julai Mosi, 2016 na Septemba 4, 2017 wakiwa Katika ofisi za NSSF makao makuu iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam mshtakiwa Njozi na Kapera kwa nia ya kufanya udanganyifu waligushi jumla ya hundi 47 za benki ya CRDB ambazo ni akaunti namba 01J1028249500 ya bodi ya wadhamini ya NSSF.

Shtaka la tatu tarehe hiyo katika ofisi za NSSF makao makuu iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa wote wakiwa watumishi wa umma walioajiliwa waliiba jumla ya zaidi ya bilioni 2 mali ya bodi ya wadhamini ya NSSF.

Simon amedai katika shtaka la nne tarehe hiyo hiyo katika ofisi za NSSF makao makuu iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam wastakiwa wote wakiwa watumishi wa umma waliisababishia hasara NSSF kiasi cha zaidi ya bilioni 2 kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Katika staka la tano tarehe hiyo hiyo katika ofisi za NSSF makao makuu iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa wote kwa pamoja walijihusisha na mihamala haramu ya zaidi ya bilioni 2 huku wakifahamu fedha hizo ni mazalio ya kosa tangulizi. Simon amedai upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Mhina alisema Washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo isipokuwa ni mahakama kuu pekee. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 15, 2014.

Updated: 01.10.2019 16:59
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.