Vijana 10 wa JKT wahofiwa kufariki ajalini

Walikuwa wakitoka kambi ya Igunga mkoani Tabora kwenda Itende, Mbeya

Vijana 10 wa JKT wahofiwa kufariki ajalini

Walikuwa wakitoka kambi ya Igunga mkoani Tabora kwenda Itende, Mbeya

14 June 2018 Thursday 19:42
Vijana 10 wa JKT wahofiwa kufariki ajalini

Zaidi ya Vijana 10 waliokuwa wakielekea kwenye mafunzo ya vitendo katika kambi ya JKT ItendeMbeya, wahofiwa kufariki dunia baada ya basi walilopanda kupata ajali eneo la mteremko wa Igodima, nje kidogo ya mji wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, Musa Talibu amesema vijana hao walikuwa wakitokea kambi ya Igunga mkoani Tabora wakielekea kambi ya mafunzo ya jeshi ya Itende, Mbeya.

Kamanda Taibu alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva aliyekuwa akiendesha gari kwa kasi bila kufuata alama za barabarani.

“Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva ambae pia ni mmoja ya waliofariki papo hapo, vijana hawa wametokea Mkoani Tabora walikuwa wanakuja Mbeya kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika kambi yetu ya Itende. Mpaka sasa hatuna tarifa kamili za idadi ya majeruhi”, alisema Taibu.

 Kamanda huyo alisema, katika gari hilo walikuwemo vijana 210 waliokuwa wanakwenda Mbeya kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika kambi ya Itende.

Keywords:
Musa Talib
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.