Vilio, simanzi, vyatawala uagaji miili wafanyakazi Azam Media

Vilio, simanzi, vyatawala uagaji miili wafanyakazi Azam Media

09 July 2019 Tuesday 14:24
Vilio, simanzi, vyatawala uagaji miili wafanyakazi Azam Media

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
VILIO, Simanzi na huzuni vimetawala leo jijini Dar es Salaam katika uagaji wa miili mitano ya wafanyakazi wa Azam Media.

Miili hiyo imeagwa katika ofisi za makao makuu ya Azam Media Tabata T.O.T ambapo wanafamilia, viongozi mbalimbali na wananchi walishiriki kutoa salamu na rambirambi zao.

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema “Azam Media mchango wake katika tasnia ya habari nchini ni mkubwa sana na hawa vijana walio mbele yetu wamechangia sana katika mafanikio haya,” 

Katibu  mkuu shirikisho la soka nchini (TFF) Wilfred Kidao amesema, “Watu huwa wanasema, msiba usikie kwa jirani, kwetu TFF, sisi ni sehemu ya msiba huu kwasababu sote tunajua ujio wa Azam TV umeleta maendeleo makubwa ya mpira wetu wa miguu''

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema “Ni sahihi kuongea kama wengine walivyotangulia, mwaka huu ni mgumu kwa tasnia ya habari na ni ushuhuda kuwa tasnia ya habari inapoguswa, nchi nzima inatikisika,” 

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema “Sisi kama chama tumepata mshituko mkubwa sana na kwenye tasnia ya habari huo ni msiba mkubwa ndani ya muda mfupi mwaka huu''
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema “Nimetafakari neno pole yangu inawezaje kuondoa majeraha kwenye familia hizi nikaona haliwezi, kwasababu mioyo ya wanafamilia, watumishi wenzake na Watanzania ambao tumefaidi matunda ya kazi zao haitaweza kuponywa na neno pole''

Mfanyakazi wa Azam Media, James Ngazi akimuelezea marehemu Salim Mhando amesema “Salim Mhando ni mtu ambaye aliyekuwa anapenda nidhamu katika kazi, Salim alikuwa kiongozi, sisemi hivyo kwasababu hatunaye leo,” – 

Amesema ''Charles alikuwa ni rafiki na mshauri, alikuwa ni kaka na mshauri mkubwa sana na alipenda kujifunza mambo mengi.”
Baada ya kuagwa watazikwa Dar es salaam, mwingine mkoani Kagera na Tanga.

Wafanyakazi wa Azam TV waliofariki kwenye ajali hiyo ni Salim Mhando (muongozaji wa matangazo), Florence Ndibalema (Mhandisi wa Sauti), Sylvanus Kasongo (Mhandisi Mitambo) na wapiga picha wawili Said Haji na Charles Wandwi.

Watu wengine wawili waliofariki ni dereva wa gari ambalo Azam TV walilikodi pamoja na msaidizi wake, Wafanyakazi watatu wa Azam TV waliojeruhiwa ni Artus Masawe, Mohammed Mwinshehe na Mohammed Mainde.

Ajali hiyo  ilitokea majira ya saa 2:30 asubuhi katika  eneo la Kizonzo katikati ya  Igunga(Taboro) na Shelui (Singida)  ambapo  basi  aina ya  Coaster lililowabeba  wafanyakazi  wa  Azam  Media  Limited  likielekea  Mwanza kugongana uso kwa na uso na Lori la  mizigo  lililokuwa   Iinakwenda   Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Azam Media limited walikuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea kwenye sherehe za uzinduzi wa hifadhi va Taifa va Burigi-Chato kwa ajili va kurusha matangazo ya moja kwa moja ya sherehe hizo.

Gari lililobeba miili ya wafanyakazi hao;

Updated: 09.07.2019 15:36
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.