Wadaiwa sugu wa kodi ya serikali hawa hapa

Wadaiwa sugu wa kodi ya serikali hawa hapa

11 June 2019 Tuesday 12:34
Wadaiwa sugu wa kodi ya serikali hawa hapa


Na mwandishi wetu, Dodoma
SERIKALI imezitaja taasisi na mashirika binafsi na ya umma ambayo ni wadaiwa  sugu wa malipo ya kodi ya ardhi na pango nchini, linaloongoza linadaiwa  zaidi ya takriban bilioni 40.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi leo Juni 11, 2019 mjini Dodoma amezitaja taasisi na mashirika  yanayoongoza kwa kudaiwa kuwa ni TTCL takribani bilioni 40, Tanesco bilioni 25.5, Narco bilioni 23.4, NBC bilioni 17.54, SUA bilioni 10.78.
Mengine ni TIC bilioni 9.19, TIAA bilioni 8, Kibaha Education Centre 5.52, Maize Production bilioni 5.43, TRC bilioni 4.19, Sido bilioni 3.5, NHC bilioni 3.41 na Mbeya Cement bilioni 3.3.
Hayo ni miongoni mwa taasisi na mashirika  takribani 207 yanayodaiwa kodi nchini.

Updated: 11.06.2019 12:43
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.