Wahariri, ACT Wazalendo waibana serikali

Wahariri, ACT Wazalendo waibana serikali

12 July 2019 Friday 10:51
Wahariri, ACT Wazalendo waibana serikali

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
KAULI 'tata' iliyotolewa na waziri Profesa Palamagamba Kabudi ya  kuwa mwandishi Azory Gwanda 'alitoweka na kufariki' imezidi kuibua hisia za wadau na sasa wanaitaka serikali itoe ufafanuzi zaidi na wa kina kuhusu suala hilo. 

Hata hivyo taarifa ya  Julai 11, 2019 ya  msemaji mkuu wa serikali, Dk Hassan Abas inaeleza "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea."

Kauli hiyo ni kufuatia Julai 10, 2019 katika mahojiano na BBC katika kipindi cha FOCUS ON AFRICA mjini London waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kikanda, Profesa Kabudi kukaririwa akisema Gwanda 'alitoweka na kufariki' Pia alisema visa vya watu kutoweka vimesababisha uchungu mwingi nchini. 

Kutokana na sintofahamu hiyo Jukwaa la wahariri nchini (TEF) imetoa mapendekezo saba huku chama cha ACT Wazalendo kikitoa mapendekezo matatu, yote yakiitaka serikali itoe majibu ya kina.

Taarifa ya TEF iliyosaniwa na kaimu mwenyekiti, Deodatus Balile inataka kujibiwa hoja hizi; 
1 Azory alikufa kifo kipi?
2  Alifia wapi?
3 Mwili wake ulizikwa, ulitupwa porini au uliyeyushwa kama wa Khashogi?
4 Prof. Kabudi amepata wapi taarifa ya kifo cha Azory?
5 Haki ya familia na waadishi wa habari kumzika na kuweka matanga itapatikanaje?
6 Je ni akina nani walimchukua Azory na kisha kumuua?
7 Je, sasa serikali inachukua hatua gani baada ya kauli hii nzito mpya ya Pro. Kabudi juu ya kifo cha Azory?
Na kwamba ''Kwa kuwa polisi walisema hawana taarifa, TEF tunaona Prof. Kabudi ni mtu sahihi sasa wa kuwapa taarifa kamili ili sasa umma ujulishwe kwa kina kilichomfika mwandishi wa habari Azory''

Nayo taarifa kwa umma iliyotolewa leo Julai 12, 2019 na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, ACT Wazalendo Ado Shaibu anaeleza msimamo wao kuwa;
1. Tunataka Jeshi la Polisi limuite na kumhoji Waziri Kabudi atoe maelezo ya wapi, lini na kwa namna gani  mwanahabari Azory Gwanda alifariki?.

2. Serikali itoe ufafanuzi wa kina kuhusu suala la Azory; nani walimteka? kwa nini walimteka? wapi alipelekwa? bado yupo hai au amefariki? Mwili wake upo wapi? 

Kama Azory amefariki, Serikali ihakikishe mwili wake unakabidhiwa kwa familia yake ili waweze kuuzika na kuweka matanga kwa mujibu wa    mila na desturi.

3. Tunatoa rai ya kuwepo kwa uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu suala la Azory Gwanda.


Naye  naibu waziri wa mambo ya ndani wa zamani, Balozi Khamis Kagasheki katika ukurasa wake wa Twitta ameandika:

Hata hivyo taarifa iliyotolewa  jana Julai 11, 2019 na Pro. Kabudi inaeleza; "Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kimakosa mahojiano yangu kwenye kipindi cha BBC FOCUS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba mwanahabari Azory Gwanda amefariki dunia."

"Hii sio tafsiri sahihi kuhusu kile nilichokisema. Katika mahojiano hayo nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa ni la kuhuzunisha na wapo watanzania waliouwawa na wengine kupotea. SIKUTHIBITISHA kuwa Azory Gwanda amefariki."

Azory Gwanda ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa kujitegemea alitoweka Novemba 21, 2017.

Alikuwa ni mmoja wa waaandishi wa kwanza kabisa kuripoti kwa kina juu ya mfululizo wa mauaji yaliyokuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana yaliyowalenga polisi na viongozi wa mji huo na kuzua hofu kubwa.

Mke wake Anna Pinoni alisema watu wapatao wanne wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe walimchukua Azory kutoka katikati ya mji, mahali ambapo hupendelea kukaa.

Anasema pia aliporudi nyumbani alikuta vitu vimezagaa, ishara kwamba inawezekana waliipekua nyumba yao.

PICHANI CHINI; Ado Shaibu ambaye ni Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, ACT Wazalendo

Updated: 12.07.2019 11:11
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.