Wahujumu uchumi wawili waliokiri wahukumiwa jela miaka 20 au kulipa faini milioni 101

Wahujumu uchumi wawili waliokiri wahukumiwa jela miaka 20 au kulipa faini milioni 101

01 October 2019 Tuesday 14:13
Wahujumu uchumi wawili waliokiri wahukumiwa jela miaka 20 au kulipa faini milioni 101

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MAGDALENA Uhwello na Halima Nsubuga wakazi wa Dar es Salaam wamehukumiwa kulipa jumla ya Sh101 milioni au kwenda jela miaka 20 baada ya kukiri mashtaka katika ya kesi uhujumu uchumi iliyokuwa ikiwakabili.

Pia dola za kimarekani 263,567 walizozitakatisha kwa kuzihamisha kwenda katika akaunti ya Smart Magaya ya Benki ya Equity, Ugànda na dola za kimarekani 124,433.89 zilizokuwa katika akaunti ya pamoja ya washtakiwa hao kwenye benki ya Equity, Dar es Salaam, zimetaifishwa na mahakama.

Hukumu hiyo imetolewa leo Oktoba 1, 2019 na Hakimu Mkazi Vick Mwaikambo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam

Akitoa hukumu hiyo, hakimu huyo amesema katika shtaka la kuendesha biashara ya upatu bila kibali, washtakiwa hao watàlipa faini ya milioni moja au jela mwaka mmoja.

Katika shtaka la pili la utakatishaji fedha, washtakiwa hao watàlipa faini ya milioni 100 au kwenda jela miaka 20.

Kabla ya kupewa adhabu hiyo, upande wa mashtaka uliwakilishwa na wakili Jackline Nyantori na Wankyo Simon, uliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa washtakiwa wengine na pia wameomba mahakama itàifishe fedha zote za upatu.

Hata hivyo, wakili wa utetezi Agustine Shio aliomba washtakiwa hao wasipewe adhabu kali kwa sababu wameipunguzia mahakama gharama za uendeshaji wa kesi kwa kuwa wamekiri mashtaka yao. Pia alidai washtakiwa hao hawapingi kutaifishwa kwa fedha zilizoombwa kutaifishwa.

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya April mosi hadi 25, 2017 katika sehemu tofauti jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa waliendesha upatu huo unaojulikana kwa jina la D9 kwa kushirikiana na mratibu wa mchezo huo kutoka nchini Ugànda aitwaye Smart Magaya.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuratibu mchezo huo nchini kwa kutafuta wanachama wapya kupitia semina na mitàndao ya kijamii kama WhatsApp na kufànikiwa kukusanya fedha dola za kimarekani 370,000.

Walikusanya fedha hizo kutoka kwa watu mbalimbali huku wakiwaahidi kupata faida zaidi, ilibainika kwamba D9 haikuwa ikiendesha bishara yeyote.

Mkurugenzi wa Makosa ya jinai nchini(DCI) alibaini mchezo huo kupitia taarifa za kiinterejensia na kufanikiwa kukamatwa kwa washtakiwa hao na kufikishwa mahakamani.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.