Waislam washeherekea Eid ul-Adha

Waislam washeherekea Eid ul-Adha

12 August 2019 Monday 07:08
Waislam washeherekea Eid ul-Adha

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

WAUMINI wa dini ya Kiislamu duniani kote wanasherehekea sikukuu ya Eid ul-Adha. Hii ni moja ya sikukuu za Eid. Baadhi ya watu, hasa wasio waumini wa dini hiyo wamekuwa wakishindwa kutofautisha kati ya Eid ul-Fitr na Eid ul-Adha.

Lakini hizi ni sikukuu tofauti.

Eid ul-Adha

Eid al-Adha ndiyo sikukuu kuu zaidi ya kidini miongoni mwa Waislamu kote duniani na pia huwa ni siku ya mapumziko mataifa mengi yenye Waislamu.

Eid al-Adha maana yake ni "sikukuu ya kutoa kafara/kuchinja" kwa Kiarabu na hutumiwa kukumbuka wakati nabii Ibrahimu alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ismail alivyoamriwa na Allah, lakini akapewa kondoo na Mungu amtoe kafara badala yake.

Sikukuu ya Eid ul-Adha huadhimishwa kuanzia siku ya 10 tangu kuonekana kwa mwezi wa Dhul Hijjah(mfungo tatu). Ibada ya Hajj kwenda Makka huanza kabla ya Eid al-Adha na tarehe yake huthibitishwa baada ya kuoenakana kwa mwezi huo wa Dhul Hijjah.

Eid al-Adha ina majina mbalimbali katika mataifa ya Kiislamu:

Eid ul-Fitr

Eid ul-Fitr maana yake ni "sikukuu ya kumaliza mfungo" na kutumiwa kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Siku hii huwa ni siku rasmi ya mapumziko katika mataifa mengi yenye waumini wengi wa Kiislamu. Hata hivyo idadi ya siku za mapumziko huwa tofauti katika nchi mbalimbali.

Waislamu huanza sherehe hizi kwa kukusanyika kwa maombi ya kila mwaka ambayo hufanyika muda mfupi baada ya machweo.

Ni kawaida kuwaona Waislamu wakikusanyika katika misikiti na viwanja vya wazi kwa swala ya pamoja.

Kabla ya ibada hiyo, huwa wanatoa sadaka kwa maskini au watu wasiojiweza(huitwa Zakat fitri) ambayo ni moja ya nguzo kuu katika dini ya Kiislamu.

Ni kawaida kwa miji mikuu mataifa ya Kiislamu kupambwa sana na sherehe kubwa kuandaliwa, watoto kununuliwa nguo mpya na kupewa zawadi mbalimbali.

Siku hii huadhimishwa baada ya kuonekana kwa mwezi wa Shawwal.

PICHANI JUU: Waislam wakiwa katika moja ya viwanja  vya wazi wakiswali swala ya Eid. Ni sunna swala hiyo kuswaliwa katika viwanja

PICHANI CHINI:Waislam wakiwa nchini Saudi Arabia  katika mji wa Makka wakikamilisha nguzo ya Hijja kati ya nguzo tano za Uislam.

Updated: 12.08.2019 07:22
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.