Wamiliki akaunti You Tube wapandishwa kizimbani

Wamiliki akaunti You Tube wapandishwa kizimbani

05 June 2019 Wednesday 14:05
Wamiliki akaunti You Tube wapandishwa kizimbani


Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
WATU wanne wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kuchapisha maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Washitakiwa hao ni Charles Kombe (24) mkazi wa Mikocheni, John Chuwa (28), mkazi wa Barakuda ,Amos Warema (27) na Raymond Mkoroka (30).

Washitakiwa hao walisomewa mashitaka hayo kwa Hakimu Mkazi Mkuu Maira Kasonde, Hakimu Mkazi,Janeth Mtega, Hakimu Mkazi Mwandamizi,Agustina Mbando na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali,Elizabeth Mkunde alidai kuwa kati ya mwaka 2018 na Aprili 20,2019 jijini Dar es Salaam Chuwa akiwa jijini Dar es Salaam alichapisha maudhui kwenye  youtube yenye jina la John filamu bila ya kuwa na kibali cha TCRA jambo ambalo ni kosa la sheria ya mtandao.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikiri shtaka linalomkabili

Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya milioni 5 kila mmoja. Kesi iliahirishwa hadi Juni 7 mwaka huu itakapotajwa tena.

Mshitakiwa Kombe alisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mmbando ambapo wakili wa serikali Elizabert Mkunde alidai alitenda kosa hilo kati ya Agosti 1 ,2017 hadi Mei 21 ,2019 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa alichapisha maudhui hayo kupitia mtàndao wake wa Youtube  uitwao Charles Kombe bila kibali.

Mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo na , upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya milioni 5  kila mmoja. Kesi iliahirishwa hadi Julai 7 mwaka huu itakapotajwa

Naye Wakili wa Serikali,Candid Nasue alisoma hati ya mashtaka na kudai kuwakati ya Novemba,2018 na Mei,2019 Francis akiwa jijini Dar es Salaam alichapisha maudhui kwenye kauti ya youtube yenye jina la Pro Media Tz bila ya kuwa na kibali cha TCRA jambo ambalo ni kosa la sheria ya mtandao.

Mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo na aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kujidhamini mwenyewe na kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya milioni 3.

Hakimu aliahirisha shauri hilo hadi Julai 4,2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakili wa Serikali,Athanas Elia alidai kuwa Mkoloka akiwa jijini Dar es Salaam alichapisha maudhui kwenye kauti yake ya  youtube bila ya kuwa na kibali cha TCRA jambo ambalo ni kosa la sheria ya mtandao.

Baada ya kusomewa shtaka hilo alikana hivyo wakili Elia alidai upelelezi haujakamilika.

Hakimu Rwezile alisema mshtakiwa anatakiwa awe na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya  milioni 5 na awe na vitambulisho na barua kutoka kwenye ofisi ya kata.

Mshitakiwa huyo yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja na kujidhamini mwenyewe kwa kusaini bondi ya  milioni 5.

Hakimu Rwezile  iliahirishwa kesi hiyo hadi Julai 4 mwaka huu itakapotajwa.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.