Wananchi wamshambulia rais wao kwa ngumi na mateke

Walipombaini kuwa ni yeye, walianza kutoa kipigo hicho hali iliyomlazimisha rais huyo  kutimua mbio huku akiomba msaada.

Wananchi wamshambulia rais wao kwa ngumi na mateke

Walipombaini kuwa ni yeye, walianza kutoa kipigo hicho hali iliyomlazimisha rais huyo  kutimua mbio huku akiomba msaada.

04 June 2019 Tuesday 08:59
Wananchi wamshambulia rais wao kwa ngumi na mateke

KATIKA hali isiyo ya kawaida raia wa nchi ya Ivory Coast waishio nchini Ufaransa, wamemshambulia kwa mateke na ngumi rais wao wa zamani,  Laurent Gbagbo.


Tukio hilo la kushangaza na la aina yake limetokea hivi karibuni jijini Paris katika moja ya mtaa ambapo rais huyo alikuwa akitembea peke yake.


Ndipo walipombaini kuwa ni yeye, walianza kutoa kipigo hicho hali iliyomlazimu rais huyo  kutimua mbio huku akiomba msaada.

Tukio hilo limesambazwa kupitia video fupi (Clip) na kumuonyesha Gbagbo akilalamika kutokana na  kitendo hicho ambapo raia hao waliokuwa na jazba  wakimpiga kwa mateke na  ngumi


Haikufaamika mara moja kama rais huyo wa zamani alijeruhiwa au la na sababu ya kupigwa kwake .

Januari 15, 2019 Mahakama ya kimataifa ya ICC ilimuachilia huru rais  huyo wa kwanza wa zamani kushtakiwa katika mahakama  hiyo.

Alishtakiwa na makosa ya uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi zilizowaacha takriban watu 3000 wakiwa wameuawa huku watu 500,000 wakiwachwa bila makao katika uchaguzi uliozongwa na utata wa 2010.

Gbagbo alikamatwa mwaka 2011 katika eneo la kujifichia la Ikulu ya rais na wanajeshi wa UN pamoja na wale wanaoungwa mkono na Ufaransa waliokuwa wakimuunga mkono mpinzani wake Alassane Ouattara.


Ghasia hizo za mwaka 2010 nchini Ivory Coast ambayo ndio mzalishaji mkubwa wa Cocoa duniani , ziliajiri baada ya Gbagbo kukataa kukubali kwamba alikuwa amepoteza katika uchaguzi huo uliozongwa na utata kwa mpinzani wake  Outtara.

Majaji wa mahakama ya ICC waliamuru kwamba alikuwa hana kesi ya kujibu kwa sababu upande wa mashtaka ulikuwa umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake

Jaji Cuno Terfusser aliyekuwa akiendesha kesi hiyo alisema kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha kwamba hotuba za Gbagbo zilihusisha ama hata kuamrisha madai ya uhalifu uliotendeka.

Wakati wa ghasia hizo kulikuwa na ghasia mbaya ambazo zilisababisha mauaji katika mji wa Abidjan uliopo kusini , huku mamia wakiuawa katika mji wa Magharibi wa Duekoue.

Waendesha mashtaka walimshutumu Gbagbo na mashtaka manne ya uhalifu dhidi ya binaadamu , mauaji, ubakaji pamoja na dhulma nyengine za kingono pamoja na vitendo vya kikatili.

Alikana mashtaka hayo ambayo alisema kuwa yalichochewa kisiasa.

Updated: 05.06.2019 06:43
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.