banner68

Wananchi wangu hawajawahi kuona gari, pikipiki wala baiskeli, adai Mbunge

Ukosefu wa barabara wasababisha magari kushindwa kufika katika baadhi ya maeneo

Wananchi wangu hawajawahi kuona gari, pikipiki wala baiskeli, adai Mbunge

Ukosefu wa barabara wasababisha magari kushindwa kufika katika baadhi ya maeneo

12 June 2018 Tuesday 10:58
Wananchi wangu hawajawahi kuona gari, pikipiki wala baiskeli, adai Mbunge

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Ludewa (CCM) Deo Ngalawa amedai kuwa kuna wananchi wa vijiji kadhaa kwenye jimbo lake ambao hawajawahi kuona gari, pikipiki wana baiskeli kutokana na kukosa barabara.

Akizungumza kwenye kipindi cha maswali na majibu bungeni leo jijini Dodoma alitaka serikali kueleza lini wanachi hao watajengewa barabara angalau kiwango cha lami.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Josephat Kandege, alisema serikali inalitambua tatizo hilo na italishughulikia.

Alimuomba mbunge huyo awaeleze wananchi wake wavute subira wakati serikali ikiendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara hizo.

Aidha Naibu waziri huyo aliwaagiza mameneja wa wakala wa barabara vijijini wa mikoa ya Pwani na Katavi kutembelea maeneo ambayo miundombinu yake imeharibiwa vibaya ili kuishauri serikali.

Hata hivyo alisdome kuwa kua barabara ya Kibii hadi Kikale mkoani Pwani yenye urefu wa kilomita 66.2 itaanza kujengwa hivi karibuni kwa kiwango cha changarawe.

Alidokeza kuwa ahadi za Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na awamu hii John Magufuli kuhusu ujenzi wa barabara kiwango cha lami maeneo mengi nchini zitatekelezwa kama zilivyopangwa.

Ni azma ya serikali kuwa ahadi zote kuhusu ujenzi wa barabara zitakelezwa ndani ya miaka mitano kuanzia sasa, aliongeza.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.