Wanane akiwemo mkemia mwandamizi wa Serikali wapandishwa kizimbani

Wanane akiwemo mkemia mwandamizi wa Serikali wapandishwa kizimbani

10 September 2019 Tuesday 07:05
Wanane akiwemo mkemia mwandamizi wa Serikali wapandishwa kizimbani

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

WATU nane akiwemo mkemia mwandamizi wa Serikali, Everlight Matinga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba likiwamo la kuingiza kemikali bila ya usajili wa bodi ya Mkemia mkuu wa Serikali.

Wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Teckno Net Scientific,Benedi Assey,Ofisa Utawala ,Wenceslaus Assey,Meneja Masoko Wifrida Assey,Ofisa Masoko na Manunuzi Salvatory Assey,Mtunza Stoo,Emanuel Assey,Samwel Mahalika na Matilda Temba.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali,Ashura Mzava mbele ya Hakimu Mkazi Vick Mwaikambo alidai kuwa kati ya Mei Mosi,2016 na Aprili 30,2017 mshtakiwa wa kwanza hadi wa saba walijihusisha na biashara ya kemikali yenye uzito wa Lita 526.50 na kilogramu 874.50 bila ya kuwa na kibali kutoka bodi ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Katika shtaka la pili katika tarehe hiyo maeneo ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam mshtakiwa wa kwanza hadi wa saba wakijua ni takwa la kisheria ya kuwa na kibali kinachotolewa na bodi ya Maabara ya Mkemia Mkuu walikutwa walijihusisha na kemikali yenye uzito wa Lita 526.50 na kilogramu 874.50

Shtaka la tatu tarehe hiyo na maeneo hayo mshtakiwa wa kwanza hadi wa sita huku wakijua takwa la kisheria walikutwa wamehifadhi kemikali mbalimbali ikiwemo Laclophenol, Aceton,Acel Acid Glacial na Tricloethylene zenye uzito wa Lita 526.50 na kilogramu 874.50.

Mzava alidai katika shtaka la nne kati ya Mei Mosi,2016 na Mei 28,2016 katika maeneo ambayo hayajulikani jijini Dar es Salaam washtakiwa hao pamoja na Mkemia wa Serikali mwandamizi walitenda kosa ovu la kula njama kwa barua kutoka kwa msajili wa viwanda na watumiaji wa kemikali huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Katika shtaka la tano kati ya Januari 28,2017 katika maeneo ya ofisi ya Mkemia wa Serikali mshtakiwa Matinga akiwa mwandamizi alighushi barua ya kuwaruhusu kufanya kazi zinazohusiana na kemikali huku akijua si kweli.

Shtaka la sita tarehe hiyo hiyo washtakiwa wote wakiwa jijini Dar es Salaam walikula njama na kuingiza kemikali hizo bila kuwa na cheti cha usajili.

Alidai kati ya Juni2,2017 washtakiwa wote kwa pamoja wakiwa eneo la Bandari ya Ami iliyopo eneo la Relini Tabata jijini Dar es Salaam waliingiza kemikali zenye uzito wa Lita 526.50 na kilogramu 874.50 bila kuwa na kibali cha usajili huku wakijua ni takwa la kisheria.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana mashtaka hayo na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi haujakamilika.

Hakimu Mkazi Mwaikambo alisema dhamana kwa washtakiwa hao ipo wazi na kwamba wanatakiwa wadhamini wawili wanaofanya kazi serikalini au binafsi na wawe na kitambulisho cha Taifa (Nida) na barua za utambulisho, na watakaosaini bondi ya milioni 10 .

Hata hivyo washtakiwa Wenceslaus,Wilfrida na Matinga walifanikiwa kupata dhamana na Benedict, Salvatory, Emanuel, Mahalila na Temba walishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo wamerudishwa mahabusu. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 23, 2019 .

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.