Wapandishwa kizimbani kwa kubadilisha fedha za kigeni

Wapandishwa kizimbani kwa kubadilisha fedha za kigeni

09 July 2019 Tuesday 14:40
Wapandishwa kizimbani kwa kubadilisha fedha za kigeni

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

WAFANYABIASHRA sita wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kubadilisha fedha za kigeni bila kibali.

Wakili wa serikali Wakyo Saimon amedai hayo leo Julai 9,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma  Shahidi wakati akiwasomea mashtka yanayowakabili.

Amewataja washtakiwa hao kuwa ni Mariamu Mpanyu (29) mkazi wa kivule,Nico Gillar (28) mkazi wa Tabata,Nicodemas Saku (42) mkazi wa Jeti lumo.

Wengine ni Abdul Ally (35) mkazi wa Tandale, Adamu Juma (42) mkazi wa Gongolamboto na Jean Bishikwabo (49) mkazi wa Tegeta.

Katika shtaka la kwanza washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kula njama ya kutenda kosa.

Imedaiwa kuwa katika tarehe tofauti zisizofahamika ndani ya Jiji la Dar es salaam washtakiwa hao walikula njama na kujihusisha na biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila kuwa na kibali.

Katika shtaka la pili washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kujihusisha na biashara ya kubadilisha fedha bila kuwa na kibali kinyume na sheria ya kubadilishaji fedha za nje.

Inadiwa kuwa kati ya Juni 18 katika mtaa wa sikukuu Kariakoo Manispaa ya Ilala washtakiwa hao walikutwa wakibadilisha fedha mbalimbali sawa na shilingi 19,528,569.3 fedha za Tanzania bila kuwa na leseni kutoka benki.

Wakyo alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko aliomba Mahakama kuwapa wateja wake  dhamana  kwakuwa mashtaka walioshtakiwa nayo yanadhaminika kwa mujibu wa sheria.

Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Shahidi alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamin wawili wenye barua na vitambulisho watakao saini bondi ya milioni 10  kila mmoja.

Washtakiwa watatu walishindwa kutimiza  masharti ya dhamana,Hakimu Shahidi ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 30 itakapotajwa tena.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.