Wapandishwa kizimbani kwa uhujumu uchumi

"Washtakiwa, wamekutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vya USD 30000 sawa na Sh. 69,025,000 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori"

Wapandishwa kizimbani kwa uhujumu uchumi

"Washtakiwa, wamekutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vya USD 30000 sawa na Sh. 69,025,000 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori"

22 May 2019 Wednesday 04:49
Wapandishwa kizimbani kwa uhujumu uchumi

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
WATU watatu, wakazi wa jijini Dar es Salaam,  wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitaka la uhujumu uchumi kwa kwa kukutwa na nyara za serikali na utakatishaji wa vipande vinne vya meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya   Milioni 69.


Wakili wa serikali Candid Nasua amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Godlisten Mtui, mfanyabiashara, Frank Lucas dereva wa pikipiki na Mhando Shomary, Mkulima


Mbele ya Hakimu Mkazi Maila Kasonde imedaiwa,  Mei 7, 2019 huko katika eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, washtakiwa, walikutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vya USD 30000 ambazo ni sawa na Sh. 69,025,000 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.


APia washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la utakatishaji,  wanadaiwa kumiliki vipande hivyo vya meno ya tembo huku wakielewa fika kuwa, vipande vivyo vya meno ya tembo vimetokana na kosa  la uwindaji haramu.


Washitakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa, mahakama ya Kisutu  haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), atakavyoelekeza vinginevyo.


Washitakiwa wote wamerudishwa rumande hadi Juni 4, 2019 kesi hiyo itakapotajwa. Upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.