Waraka kufupisha muda wa mashauri ya walimu waja, Bunge laambiwa

Serikali itatoa maelekezo hivi karibuni ili kuhakikisha kuwa mashauri hayo yanasikilizwa kwa muda mfupi

Waraka kufupisha muda wa mashauri ya walimu waja, Bunge laambiwa

Serikali itatoa maelekezo hivi karibuni ili kuhakikisha kuwa mashauri hayo yanasikilizwa kwa muda mfupi

06 June 2018 Wednesday 17:27
Waraka kufupisha muda wa mashauri ya walimu waja, Bunge laambiwa

Na Mwandishi Wetu

SERIKALi imesema itatoa waraka kuhimiza usikilizaji haraka wa mashitaka ya walimu ili kuwafanya waendelee kulitumikia taifa badala ya kesi.

Hayo yameelezwa bungeni leo na Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Kakunda wakati akijbu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbulu Mjini Paul Isaay (CCM).

Mbunge huyo alisema kuwa mashitaka mengi ya walimu yanachukua muda mrefu sana na kuna umuhimu kwa serikali kutoa waraka maalum ili kufupisha.

Akijibu Naibu Waziri Kakunda, alikiri kuwa ni kweli kuna maeneo ambapo mashauri hayo yanachukua muda mrefu kutokana na mambo yanayohitajika.

Hata hivyo alisema kuwa kuna mashauri mengine hayahitaji ushahidi mwingi na yanaweza kutolewa na mkuu wa shule husika.

Alidokeza kuwa serikali itatoa maelekezo hivi karibuni ili kuhakikisha kuwa mashauri hayo yanasikilizwa kwa muda mfupi.

Akijibu swali la Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa (CCM) aliyetaka kujua lini waalimu waliohamishiwa shule za msingi kutoka sekondari watalipwa, Naibu Waziri alisema kuwa suala lao linashughulikiwa.

Mbunge huyo alisema kuwa wilaya ya Karagwe ina walim 51 ambao walikuwa wanafundishwa sekondari na sasa wapo shule za msingi lakni bado hawajalipwa stahiki zao.

Akijibu, Kakunda alisema kuwa tayari Rais John Magufuli alitoa maagizo kuwa watumishi wote wanaohamishwa walipwe kwanza kabla ya uhamisho.

Hata hivyo alidokeza kuwa walimu hao wa Karagwe na wengineo waliohamishwa kabla ya agizo la Rais watalipwa fedha zao.

Aliwataka kuwa na subira na kuongeza kuwa serikali inashughuliikia na watalipwa mwaka wa  fedha  ujao.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.