Wasambazaji picha za marehemu mitandaoni sasa kukamatwa

Wasambazaji picha za marehemu mitandaoni sasa kukamatwa

14 August 2019 Wednesday 13:39
Wasambazaji picha za marehemu mitandaoni sasa kukamatwa

Na mwandishi wetu, Morogoro

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wote wanaosambaza picha za marehemu katika mitandao ya kijamii.

Ametoa agizo hilo leo Agosti 14, 2019 mkoani Morogoro na kwamba usambazaji huo wa picha ni kosa kisheria.
 

“Kusambaza picha za marehemu katika mitandao ya kijamii ni kuwadhalilisha wahusika na ni uvunjaji wa sheria za nchi. Ninaziagiza mamlaka na vyombo vinavyohusika vihakikishe vinafuatilia na kuchukua hatua kwa wale ambao wanakiuka sheria za nchi kwa kusambaza mitandaoni picha za marehemu,” amesema Masauni.

Amesema si vizuri kutumia majanga ya kitaifa kama ajali ya moto iliyotokea Msamvu Morogoro na kusababisha zaidi ya watu 80 hada sasa kufariki dunia na kusambaza picha za waathirika kwa dhamira ya kudhalilisha .

“Watu hawa wamefariki dunia na mtu yeyote katika tukio lile angekufa, mimi au wewe, ndugu yako au jamaa yako, fikiria kama ni jambo limekukuta au ndugu yako halafu ukachukua picha na kuisambaza kwenye mitandao, katika mazingira kama yale,” amesema naibu waziri huyo.


 

Updated: 14.08.2019 13:50
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.