Watanzania milioni 5 wanamiliki vitambulisho vya uraia

Watanzania milioni 5 wanamiliki vitambulisho vya uraia

12 June 2019 Wednesday 10:43
Watanzania milioni 5 wanamiliki vitambulisho vya uraia

Na mwandishi wetu, Dodoma
SERIKALI imesema hadi mwishoni  mwa mwezi Desemba 2019, takribani watanzania milioni 22.2 watakuwa wameandikishwa na kupata vitambulisho vya uraia na kwamba  ni watanzania milioni 5 ndio wanaomiliki vitambulisho hivyo hadi sasa.


Idadi hiyo imeelezwa leo Juni 12, 2019 Bungeni Dodoma na Naibu waziri wa Mambo ya Ndani  Hamad Yusuf Masauni.


Amesema hadi sasa ni watanzania milioni 5 ndio wanaomiliki vitambulisho vya uraia na vitambulisho milioni 13 vipo katika hatua ya mwisho kukabidhiwa kwa watanzania.


"Takwimu zilizopo ni milioni 5 ndio wenye vitambulisho vya uraia, vitambulisho milioni 13 vipo katika hatua ya mwisho kukabidhiwa watanzania. Na ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba 2019 jumla ya watanzania milioni 22.2 watakuwa na vitambulisho vya uraia," amesema naibu waziri huyo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.