Watatu wafariki kwa kupigwa risasi, askari ajeruhiwa

Watatu wafariki kwa kupigwa risasi, askari ajeruhiwa

23 July 2019 Tuesday 11:07
Watatu wafariki kwa kupigwa risasi, askari ajeruhiwa

Na mwandishi wetu, Mwanza
TAKRIBANI watu wanne wamefariki na wawili wamejuruhiwa kwenye vurugu zilizotokea katika kisiwa cha Sizya, wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewataja waliofariki kuwa ni wananchi watatu kwa kupigwa risasi na afisa ulinzi wa rasilimali kwa kushambuliwa na wananchi. Waliojeruhiwa ni askari polisi na mwananchi mmoja ambao wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Nansio.

Amesema tukio hilo limetokea mchana wa Julai 22, 2019 baada ya kutokea mzozo na mvutano kati ya wataalam, kikosi cha kudhibiti uvuvi haramu na wananchi.

''Taarifa za awali ni kuwa watu wanne walipigwa risasi, watatu walifariki hapo hapo, mmoja alijeruhiwa. Pia  kiongozi wa kikosi cha ulinzi wa rasilimali aliuawa na wananchi na mmoja wa askari polisi amejeruhiwa vibaya. Majeruhi wote wapo katika hospitali ya Nansio,'' amesema  na kuongeza

"Tukio hili limetokea mchana katika kisiwa cha Sizya karibu na kisiwa kikubwa cha Ghana Ukerewe, kulikuwa na doria ya kupambana na uvuvi haramu. Ndipo kukatokea mzozo na mvutano kati ya wataalam, kikosi cha kudhibiti uvuvi haramu na wananchi''

Mongella ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo amekemea kitendo hicho na kwamba  uchunguzi unaendelea kuthibitisha chanzo  nini na nani ni chanzo.

"Kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo ipo eneo la tukio na leo Julai 23, kamati ya mkoa nayo itafika eneo la tukio,'' amesema

Updated: 23.07.2019 11:18
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.