Watu 10 matajiri zaidi kuwahi kuishi duniani.

Watu 10 matajiri zaidi kuwahi kuishi duniani.

11 June 2019 Tuesday 17:37
Watu 10 matajiri zaidi kuwahi kuishi duniani.

KULINGANA na orodha ya jarida la Forbes la 2019 iliotolewa wiki hii, mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos ndiye mtu tajiri zaidi duniani

Akiwa na mali yenye thamani ya $131bn (£99bn) ndiye mtu tajiri zaidi duniani.

Lakini yeye sio mtu tajiri kuwahi kuishi duniani. Taji hilo linadaiwa kumilikiwa na Mansa Musa , mfalme wa karne ya 14 kutoka Afrika Magharibi ambaye utajiri wake ungeathiri uchumi wa taifa zima.

Akaunti zake zilikuwa na utajiri mkubwa kitu ambacho ilikuwa vigumu kuweza kubaini thamani ya utajiri na uwezo wake ,kulingana na Rudolph Butch profesa wa Historia katika chuo kikuu cha California .

Mansa Musa alikuwa tajiri zaidi ya mtu yeyote angeweza kuelezea, Jacob Davidson aliandika kuhusu mfalme huyo wa Afrika katika tovuti ya Money.com mwaka 2015.

Mwaka 2012 Tovuti ya Marekani iliweka thamani yake kuwa $400bn, lakini wanahistoria wa kiuchumi wanakubaliana kwamba mali yake haikuweza kuhesabiwa kwa kutumia nambari.

Watu 10 matajiri zaidi kuwahi kuishi duniani.

  • Mansa Musa (1280-1337, Mfalme wa Mali ambaye mali yake haiwezi kuelezewa
  • Augustus Caesar (63 BC-14 AD, Mfalme wa Roma ) $4.6tn (£3.5tn)
  • Zhao Xu (1048-1085, Mfalme wa Shenzong of Song China) mali yake haikuweza kuhesabika
  • Akbar I (1542-1605, Mfalme wa Mughal India) mali yake haikuweza kuhesabika
  • Andrew Carnegie (1835-1919, Mfanyabiashara wa viwanda wa Uskochi na Marekani ) $372bn
  • John D Rockefeller (1839-1937) Mfanyabishara wa Marekani ) $341bn
  • Nikolai Alexandrovich Romanov (1868-1918, Tsar wa Russia) $300bn
  • Mir Osman Ali Khan ( 1886-1967, Ufalme wa India ) $230bn
  • William The Conqueror (1028-1087) $229.5bn
  • Muammar Gaddafi (1942-2011, -Mtawala wa Libya) $200bn

Chanzo: Money.com, thamani ya watu maarufu

Updated: 12.06.2019 17:27
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.