Watu 60 wafariki dunia katika ajali

Watu 60 wafariki dunia katika ajali

10 August 2019 Saturday 12:43
Watu 60 wafariki dunia katika ajali

Na mwandishi wetu, Morogoro
TAKRIBANI watu 60 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kulipuka leo Agosti 10, 2019 katika eneo la Msamvu mjini Morogoro.

Kamanda wa Polisi wa Morogoro, Wilbroad Mtafungwa amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba  inahofiwa kuna miili mingine ambayo imebanwa chini ya lori hilo baada ya moto kulipuka.

Bado mamlaka husika hazijathibitisha chanzo cha ajali hiyo, lakini inadaiwa wengi wa waliopoteza uhai walikuwa wakijaribu kuchota mafuta kutoka kwenye lori hilo.

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema waendesha piki piki(bodaboda) ndio walioathirika zaidi.

Picha zilizo chapishwa katika mitando ya kijamii zinaonesha miili kadhaa ya watu iliyoteketea kupita kiasi ikiwa imetapakaa katika eneo la tukio.

Mmoja wa manusura amesema "Hapa nilikuta watu wanang'ang'ania mafuta na watu walikuwa bizee kuchota mafuta na hawaelewi haya ni mafuta au maji. Katika huo mshangao sasa mimi nasikia moto umelipuka. Moto ulipozuka tukaanza kukimbiana, kila mmoja anajiokoa kivyake vyake, kufikia hapo nimeanguka chini nikaanza kutambaa kwa magoti nikafanikiwa kuondoka ."
Morogoro ni moja ya njia kuu za malori yanayobeba shehena ya mizigo na mafuta kutoka bandari ya Dar es Salaam.

Bado haijafahamika lori hilo lilikuwa linamilikiwa na kampuni gani ya usafirishaji na iwapo lilikuwa linaenda nje ya Tanzania ama la.

Updated: 10.08.2019 12:55
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.