Watumishi wizara ya kilimo wapandishwa kizimbani

Watumishi wizara ya kilimo wapandishwa kizimbani

09 September 2019 Monday 14:38
Watumishi wizara ya kilimo wapandishwa kizimbani

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) imewafikisha katika Mahakama ya wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wafanyakazi wawili wa Wizara ya Kilimo, Flora Martin (49) na Prisca Joseph (33) kwa kupokea rushwa ya Sh 100,000.

Akiwasomea shtaka hilo leo Sepyemba 9, 2019, Wakili wa Takukuru, Sophia Gura amedai kati ya Januari Mosi na Agosti 31,2019 washtakiwa hao wakiwa waajiliwa wa Wizara ya Kilimo kama wakaguzi wa mazao bandarini walipokea rushwa ya Sh100,000.

Gura amedai mbele ya Hakimu Mkazi Flora Mjaya kuwa washtakiwa hao walipokea kiasi hicho cha Fedha kutoka kwa Tonny Joseph kama kishawishi cha kuwawezesha kumsaidia kwa kuruhusu mizigo yake bila kikwazo chochote.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa hao ambao wanatetewa na wakili Mkama Kalebu walikana na upande wa mashtaka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Mjaya katika kesi hiyo ya jinai namba 607/2019 alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 500,000.

Hata hivyo mshtakiwa Prisca alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa huru huku mwenzake akishindwa kuyakamilisha na kupelekwa rumande. Kesi imeahirishwa hadi Septemba 19, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.