Waziri ahimiza uanzishwaji viwanda vya pembejeo

Waziri ahimiza uanzishwaji viwanda vya pembejeo

18 June 2019 Tuesday 13:55
Waziri ahimiza uanzishwaji viwanda vya pembejeo

Na mwandishi wetu, Mbeya
WAZIRI  wa Kilimo, Japhet Hasunga amewaagiza wakuu wa mikoa ya Nyanda za Juu kusini kutenga maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya pembejeo za kilimo ili kuwaepusha wakulima wa mboga mboga na matunda  kununua mbegu bandia ambazo  zinachangia kuzorotesha uzalishaji.

Ametoa agizo hilo leo Juni 18, 2019 mkoani Mbeya kwenye kongamano la biashara na uwekezaji linaloendelea.

Limeandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mpango wa uendelezaji Kilimo Eneo la Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) na Umoja wa wakulima wa Mbogamboga na Matunda (TAHA).

Amesema kwa sasa kilimo cha mbogamboga hakina tija lakini jitihada zikifanyika hali hiyo  itabadilika na wakulima watapata manufaa.

Naye Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga mboga na kuutumia uwanja wa ndege wa Songwe kusafirishia mazao yao

Updated: 19.06.2019 09:43
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.