Waziri kuzisaka 'bodaboda' vituo vya polisi

Waziri kuzisaka 'bodaboda' vituo vya polisi

17 June 2019 Monday 10:57
Waziri kuzisaka 'bodaboda' vituo vya polisi

Na mwandishi wetu, Dodoma

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema ataanza msako katika vituo vya polisi nchini kote kukagua pikipiki(bodaboda) zilizokamatwa na kuzuiliwa kiuonevu.

Ametoa msimamo huo leo Juni 17, 2019 Bungeni Dodoma na kwamba atafanya msako huo kwa kushtukiza katika vituo hivyo.

Amesema pamoja na madereva wengi wa bodaboda kuwa na makosa mengi lakini wapo wanaokamatwa na pikipiki zao kuzuiliwa katika vituo kwa uonevu.

“Nimeshawaambia wakuu wa polisi kuwa ifikapo Julai 15, 2019 nitaaanza msako wa kushtukiza katika vituo vya polisi pamoja na mambo mengine kukagua bodaboda zilizozuiliwa kiuonevu,’’ amesema waziri huyo.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imetoa ajira ikiwemo binafsi ya uendeshaji bodaboda hivyo kukamata na kuzuia vitendea kazi hivyo ni pigo kwa waliojiajiri.

Updated: 17.06.2019 11:04
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.