Waziri Lugola aziweka mtegoni kampuni binafsi za ulinzi

Waziri Lugola aziweka mtegoni kampuni binafsi za ulinzi

19 July 2019 Friday 14:40
Waziri Lugola aziweka mtegoni kampuni binafsi za ulinzi

Na mwandishi wetu, Mara
WAZIRI  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kutokana na changamoto zilizopo katika makampuni binafsi ya ulinzi nchini, Serikali inakaribia kukamilisha sheria itakayosimamia utendaji ikiwemo suala la ajira kwa askari wa kampuni hizo.

Pia amesema serikali  haitasita kufuta kampuni hizo zinazoajiri  askari vikongwe na wasiokuwa na mafunzo ya mgambo wala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Lugola ametoa msimamo huo mapema leo Julai 19, 2019 katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika kata ya Nansimo, jimbo la Mwibara, wilayani Bunda Mkoani Mara.

Amesema kutokana na upungufu wa askari, serikali iliruhusu kuwepo kwa kampuni binafsi za ulinzi ili kusaidia ulinzi na usalama lakini baadhi ya kampuni zinavunja sheria kwa kuajiri walinzi wasiokuwa na mafunzo yoyote.

"Kutokana na changamoto hii, serikali inakaribia kukamilisha sheria  ya kampuni  binafsi za  ulinzi itakayosimamia vizuri kampuni zote nchini, na sheria hiyo itaenda kudhibiti pia masuala ya ajira  za askari wao'' amesema Lugola ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mwibara kwa tiketi ya CCM.

Amesema wizara yake haiwezi kucheza na masuala ya ulinzi na usalama kwa kuziacha kampuni kuendelrea kuajiri vikongwe ambao anadai  hawawezi kushika silaha za moto.

"Pia vikongwe hawa mara kwa mara wanasinzia kiasi kwamba muda wowote wanaweza wakanyang’anywa silaha na majambazi ambao wanazitafuta kwa ajili ya kufanyia uhalifu'' amesema

Updated: 19.07.2019 14:49
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.