Waziri mkuu aongoza kuaga miili waliofariki ajali ya moto

Waziri mkuu aongoza kuaga miili waliofariki ajali ya moto

11 August 2019 Sunday 11:45
Waziri mkuu aongoza kuaga miili waliofariki ajali ya moto

Na mwandishi wetu, Morogoro
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, viongozi wengine na wakazi wa mji wa Morogoro wamejitokeza asubuhi hii katika viwanja Shule ya Sekondari ya Morogoro kuaga baadhi ya miili ya waliopoteza maisha katika ajali ya moto ya lori la mafuta iliyotokea jana mkoani humo.

Tayari rais John Magufuli ametoa siku tatu za maombolezo kuanzia jana Agosti 10 kufuatia vifo vya zaidi ya watu 60 vilivyosababishwa na ajali  hiyo

Marehemu walikuwa wakichota mafuta yaliomwagika baada ya lori la mafuta kupinduka mjini Morogoro.

Takriban watu 70 walijeruhiwa na wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Morogoro na  ya Muhimbili  jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waliofariki wanatarajiwa kuzikwa leo Agosti 11, 2019 siku ya Jumapili. Katika kipindi chote cha maombolezo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Updated: 11.08.2019 11:59
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.