Waziri Mpango:Mabenki, taasisi za fedha ondoeni mikopo chechefu

Waziri Mpango:Mabenki, taasisi za fedha ondoeni mikopo chechefu

10 July 2019 Wednesday 14:34
Waziri Mpango:Mabenki, taasisi za fedha ondoeni mikopo chechefu

Na mwandishi wetu, Dodoma
“RIBA katika benki zetu bado ni kubwa taasisi za fedha zione namna ya kuzipunguza sambamba na kutoa mikopo kwa kuzingatia kanzidata ya wakopaji ili kuepuka mikopo chechefu.”, amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.

Amesema hayo leo Julai 10, 2019 jijini Dodoma alipokuwa  akipokea hundi ya kifani ya gawio la  bilioni moja kutoka benki ya Posta Tanzania(TPB). Alikabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo Dk Edmund Mndolwa.

Akizungumza katika hafla hiyo Dk  Mpango aliipongeza Benki hiyo kwa kutoa gawio kwa Serikali, na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.

“Utoaji huu wa gawio ni kiashiria tosha kwa Serikali kuwa Benki inazidi kukua na kuwapa moyo watanzania na wawekezaji kuwa TPB inatoa huduma bora katika jamii”, alisema Dk. Mpango.

Aliitaka Benki hiyo kuongeza wigo wa utoaji huduma ili kuwafikia wananchi hususani waishio vijijini pamoja na kutoa elimu kwa wananchi hao kuhusu umuhimu wa  kuweka akiba, kukopa sambamba na kurejesha mikopo kwa wakati.

Aidha, Dkt. Mpango ameiagiza Benki hiyo kuendelea kuwapa wanawake  kipaumbele katika upatikanaji wa huduma za fedha na mikopo ili waweze kuendesha shughuli za maendeleo.

Pia Dk Mpango aliiagiza  TPB kusimamia uadilifu kwa watumishi wake na kuwa makini na kutoa taarifa za  miamala yenye mashaka ili kuzuia utakasishaji wa fedha haramu.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Dk Edmund Mndolwa alisema kuwa gawio hilo ni sehemu ya faida ya  bilioni 17.2 kabla ya kodi ambayo Benki yake imeipata katika mwaka wa fedha 2018/19. 

Pia ameeleza kuwa Benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora ili kukidhi mahitaji ya wanahisa wake na wananchi kwa ujumla.

Aidha, Dk Mndolwa aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa utendaji mzuri ambao umeiwezesha Benki hiyo kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kuahidi kuendelea kushirikiana nayo ili kukuza uchumi wa nchi. 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.