Waziri wa zamani wa JK aachiwa kwa dhamana

Waziri wa zamani wa JK aachiwa kwa dhamana

27 May 2019 Monday 16:20
Waziri wa zamani wa JK aachiwa kwa dhamana

Na mwandishi wetu, Singida

HATIMAYE Jeshi la Polisi  mkoani Singida limemuachia kwa dhamana aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii,  Lazaro Nyalandu  pamoja na  makada wenzake wawili.

Afisa habari wa Chadema,Tumaini Makene ameiambia Azaniapost kuwa Nyalandu ameachiliwa kwa dhamana majira ya mchana Mei 28, 2019.

" Nyalandu na wenzake wawili wameachiwa kwa dhamana majira ya saa saba mchana leo Mei 28,2019," amesema Makene

Amesema kuwa  wameachiwa kwa masharti ya kila mmoj kuwa na wadhamini wawili na kila mdhamini aweke dhamana ya milioni 5.

Pia wametakiwa kurejea  kesho Mei 29, 2019 kituo kikuu cha polisi cha Singida saa mbili asubuhi wakiwa na wadhamini wao

Hatua hiyo inakuja baada ya jana Takukuru kumhoji Nyalandu,  David Jumbe ambaye ni mwenyekiti wa kata ya Itaja na Peter Mwangu ambaye ni mwenyekiti wa kijiji  kwa tuhuma za rushwa na kufanya mikutano isiyoruhusiwa.

Nyalandu ambaye alikuwa waziri katika serikali ya awamu ya nne chini ya rais mstaafu Jakaya Kikwete na alikuwa mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini kupitia CCM, alijiuzulu wadhifa wake huo na kujiunga na  Chadema.

Updated: 28.05.2019 14:54
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.