Waziri wa zamani wa JK afariki dunia

Waziri wa zamani wa JK afariki dunia

11 September 2019 Wednesday 15:54
Waziri wa zamani wa JK afariki dunia

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa bodi ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Dk Omari Nundu(71) amefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa na hospitali ya Taifa Muhimbili inasema kuwa Nundu alifikishwa hospitalini hapo leo kwa gari binfsi akiwa amefariki.

‘‘Ndipo jamaa waliokuja na mwili wake wakaamua waende kuhuifadhi mwili wake katika hospitali ya rufaa ya jeshi la Lugalo,’’ inaeleza taarifa kutoka ofisi ya uhusiano Muhimbili

Awali kabla ya kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo , alikuwa mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL) lakini Juni 12, 2019 Rais John Magufuli alimteua Mohamed Abdalallah Mtonga kushika wadhifa huo

Uteuzi wa Nundu ulifuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali na kampuni ya Bharti Airtel International juu ya uendeshaji wa Airtel Tanzania na kwamba mwenyekiti wa bodi atateuliwa na serikali.

Nundu katika uhai wake amewahi kuwa Mbunge wa Tanga na Waziri wa Uchukuzi katika serikali ya awamu ya nne rais mstaafu Jakaya Kikwete

Updated: 11.09.2019 15:59
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.