banner68
banner58

Wizara yaguswa na gogoro la muda mrefu kuhusu pori la Selous

Wananchi hawakubaliani na uhakiki wa mpaka na wanadai bwawa la Kidungulila lipo sehemu yao

Wizara yaguswa na gogoro la muda mrefu kuhusu pori la Selous

Wananchi hawakubaliani na uhakiki wa mpaka na wanadai bwawa la Kidungulila lipo sehemu yao

13 June 2018 Wednesday 12:21
Wizara yaguswa na gogoro la muda mrefu kuhusu pori la Selous

Na Mwandishi wetu

WIZARA ya Maliasili na Utalii itakutana na uongozi wa mkoa wa Lindi kutatua mgogoro wa muda mrefu kuhusu ardhi baina ya wanakijiji kimoja wilayani Liwale na hifadhi ya Pori la Selous.

Hayo yameelezwa bungeni leo na Naibu waziri wa wizara hiyo Japhet Hasunga wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Hamida Mohammed Abdallah (CCM).

Mbunge huyo alisema kuwa mgogoro huo umechukua hatua kubwa na kuitaka serikali kueleza lini itautatua.

Akijibu Naibu waziri Hasunga alisema kuwa kjiji cha Mkundungu kinapakana na pori la hifadhi la Selous, ambapo hapo awali wananchi walikuwa wakivua samaki ndani ya eneo la hifadhi.

Alisema kuwa mwaka 1982 serikali ilizuia uvuvi huo kwani walikuwa wanatumia sumu na kuwa kuna mpaka ambao umewekwa kisheria kutenganisha eneo hilo.

Alisema kuwa wananchi hawakubaliani na uhakiki wa mpaka na wanadai bwawa la Kidungulila lipo sehemu yao.

Aliongeza kuwa katika kutatua hilo, uongozi wa wizara utakutana na ule wa mkoa wa Lindi ili kuushughulikia kabla ya mwezi wa tisa mwaka huu na kumaliza kabisa tatizo.

Aidha alidokeza kuwa kumekuwapo na changamoto nyingi za mipaka na kuanzia mwezi Julai mwaka huu Wizara kwa kushiirikiana na taasisi za hifadhi itapitia upya maeneo yoe na tayari bajeti kwa ajili ya suala hilo imekwisha tengwa.

Kuhusu msitu wa nyuki uliopo maeneo ya Segerea jijini Dar es Salam alisema kuwa bado unamikiliwa na wizara na umeachwa kwa muda mrefu ili kurudisha uoto wa asili.

Alisema kuwa msitu huo pia unasaidia kupunguza hewa chafu inayosambazwa na viwanda vya jiji , na kuahidi kuwa serikali itaendelea kuutazama.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.