Yaliyomkuta Kubenea wa Chadema sasa yampata Mbunge mwingine bungeni leo

Adaiwa kuuliza swali la udini

Yaliyomkuta Kubenea wa Chadema sasa yampata Mbunge mwingine bungeni leo

Adaiwa kuuliza swali la udini

07 June 2018 Thursday 11:51
Yaliyomkuta Kubenea wa Chadema sasa yampata Mbunge mwingine bungeni leo

NAIBU Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson amelikataa swali la kidini lililoulizwa na Mbunge wa Vunjo James Mbatia (NCCR –Mageuzi) Bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.

Katika swali lake Mbunge huyo alisema kuwa jamii ikiwa na migogoro hata nchi inakuwa haina ustawi na kuwa Katiba ya Jamhuri wa Muungano imetoa haki kwa taasisi za kidini na wadau wa maendeleo kuganya kazi zao.

Alisema kuwa hivi karibuni kuna barua zilikuwa zinasambazwa za kulitaka kanisa la Kiinjili la Kilutheril Tanzania (KKKT) na la Katoliki kufuta waraka wa pasaka na Kwaresma walioutoa na akataka kusikia kauli ya serikali.

Kabla ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hajaruhusiwa kujibu, ndipo Naibu Spika Tulia akasema kuwa tayari Spika wa Bunge Job Ndugai alikwisha tolea ufafanuzi kuhusu maswali ya kidini.

Alisema kuwa swali la kidini liliwahi kuulizwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema) lakini Spika Ndugai akalikataa.

Alisema kuwa swali hilo la Mbunge Mbatia haliwezi kujibiwa na Waziri Mkuu huku akimwita Mbunge mwingine kuuliza.

Mbunge wa Timbe, Rashid Ali (CUF) alitaka serikali kueleza njia mbadala za kupunguza umasikini kwa wakulima.

Alitaka kujua kama serikali itakuwa tayari kuwa na mjadala wa kitaifa kwa ajili ya kupunguza umasikini.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa inatambua umuhimu wa wakulima kwani kuna zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanashukulika na sekta hiyo.

Alisema kuwa upo mkakati wa kuboresha kilimo kwa ajili ya chakula na biashara.

Majaliwa alikiri kuwa kua mapungufu fulani Fulani kwa kutofikia malengo ya kuzalisha.

Alidokeza kuwa wiki hii serikali ilizindua awamu ya pili ya mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo wenye lengo la kuongeza tija kwa taifa na wakulima nchini.

Kuhusu kuwepo kwa mjadala wa kitaifa kuzungumzia masuala ya kilimo alisema ni jambo jema na serikali imelipokea.

Hata hivyo Majaliwa alisema kuwa serikali itakuwa inaendelea kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza kwenye sekta hiyo nyeti kwa nia ya kuinua pato la taifa.

Azania Post

Updated: 07.06.2018 15:48
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.