Zitto: Serikali imepoteza bilioni 430

Zitto: Serikali imepoteza bilioni 430

26 July 2019 Friday 11:39
Zitto: Serikali imepoteza bilioni 430

Na mwandishi wetu, Da es Salaam

MBUNGE wa Kigoma mjini(ACT Wazalendo ), Zitto Kabwe amesema kati ya mwaka 2017- 2019 serikali imepoteza kiasi kikubwa cha makusanyo ya fedha katika sekta ya madini.

Amesema katika katika kipindi cha miaka miwili mapato ya serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka kwa TZS 430 bilioni.

"Mwaka 2016 mapato yalikuwa TZS 1.3 trilioni , mwaka 2018 mapato yalikuwa TZS 867 bilioni hivyo katika miaka 2, mapato ya serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka kwa TZS 430 bilioni''.amesema
 

Taarifa ya kiongozi huyo aliyoitoa leo Julai 26, 2019 inaeleza;

Nchi imepoteza mno kwenye sakata la Makanikia [ Fedha za kigeni $200M na TZS 430B Mapato ya Serikali]

- mwaka 2016 Tanzania iliuza nje dhahabu iliyoingiza USD 1.8 bilioni 
- Mwaka wa Makanikia 2017 mauzo nje yalishuka mpaka USD 1.6 bilioni na;
- Mwaka 2018, mwaka ambao athari ya Makanikia ilikuwa mwaka mzima mauzo nje yalikuwa USD 1.4 bilioni 

Kati ya mwaka 2017-2018 Mauzo nje ya dhahabu yalishuka kwa jumla ya $200M saw na 11%. 

Katika kipindi hicho uzalishaji wa dhahabu ulishuka kutoka tani 43 za dhahabu mwaka 2015 mpaka tani 39 mwaka 2018. Uzalishaji wa mwaka 2018 ulikuwa sawa na uzalishaji wa mwaka 2010. 

Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka katika kipindi cha Makanikia. Kwa mujibu wa Kitabu cha Mapato ya Serikali kwa Wabunge ( Revenues Book Vol. 1 ). 

- mwaka 2016/17 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 341 bilioni 
- Mwaka 2017/18 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 230 bilioni 
- Mwaka 2018/19 makusanyo yalikuwa TZS 220 bilioni.
Serikali imekadiria kukusanya TZS 350 bilioni mwaka 2019/2020. 

Kwa mujibu wa Dkt. Genuine Martin kwenye mada yake kwa Policy Forum Breakfast Debate Julai, 2019 Mapato yote ya sekta ya Madini yameshuka kwa 32% katika zama za Makanikia. 

- mwaka 2016 Mapato yalikuwa TZS 1.3 trilioni 
- Mwaka 2018 Mapato yalikuwa TZS 867 bilioni. 
Katika Miaka 2 Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka kwa TZS 430 bilioni. 

Tunapata nini kutoka Barrick Gold baada ya sakata la Makanikia? 

Mapato ambayo Serikali ya Magufuli imepoteza kwenye sekta ya Madini kati ya mwaka 2017 - 2019 ni makubwa zaidi ya malipo* ambayo Serikali inasema tutalipwa na Barrick Gold Corporation ili kumaliza mgogoro baina ya Kampuni ya Acacia na Serikali. 

Tumeona hapo juu kuwa tumepoteza Mapato ya Fedha za kigeni $200M na Mapato ya Serikali kushuka kwa TZS 430 bilioni. Kutoka Barrick tunatarajiwa kupata $300M ambazo chache kulinganisha na kiasi tulichopeteza. 

* Malipo yenyewe hayo ya $300M kwanza yatalipwa kwa miaka 7, pili yana masharti ya wao kulipwa kwanza Fedha zao za VAT ( $240M ), na tatu watasamehewa Kodi ya Capital Gains Tax ya mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick Gold ($85.6M). Hatimaye Tanzania ndio itakuwa imeilipa Barrick $25M ( Net of payments and receipts to and from Barrick Gold ). 

Kwa hiyo Tanzania imepoteza Mapato iliyokuwa yakusanywe kama mgogoro usingekuwepo [ $200M exports revenues and $170M tax revenues ] na imeishia kuilipa Barrick badala ya yenyewe kulipwa. 

Tumepata hasara kubwa sana kutokana na maamuzi yetu wenyewe, maamuzi ambayo hayakuzingatia maslahi ya nchi yetu. Tunapaswa kuwawajibisha waliotupa hasara hiyo.

Updated: 26.07.2019 12:00
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.