banner68
banner58

Zuio la kuuza chakula nje bado lipo pale pale, Waziri Mahiga aliambia Bunge

Hayo yameelezwa Bungeni leo na Waziri wa Mambo ya Nje Dk Augustine Mahiga

banner57

Zuio la kuuza chakula nje bado lipo pale pale, Waziri Mahiga aliambia Bunge

Hayo yameelezwa Bungeni leo na Waziri wa Mambo ya Nje Dk Augustine Mahiga

16 May 2018 Wednesday 18:40
Zuio la kuuza chakula nje bado lipo pale pale, Waziri Mahiga aliambia Bunge

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kuwa bado imezuia wakulima na wafanyabiashara kusafirsha chakula nchi jirani wakati taifa linakabiliwa na upungufu wa chakula.

Hayo yameelezwa Bungeni leo na Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Uhusiano wa Kimataifa Dk Augustine Mahiga, wakayi akijibu swali la Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (CUF).

Mbunge huyo alitaka kujua maana ya kauli mbiu ya Wizara ya kukuza biashara Afrika Mashariki ina maana gani huku ikiwazuia wakulima kuuza bidhaa zao nje.

Alisema mwaka jana serikali ilitoa katazo la muda kusafirisha mazao, lakini hadi sasa linaonekana kuwa ni la kudumu.

Akijibu Waziri Mahiga alisema kuwa zuio hilo la chakula linatokana na upungufu uliopo akisema wakulima wanapaswa kuuza mazao yako katika Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA).

“Serikali ina mpango wa kujenga maghala zaidi ya kuhifadhia chakula ambacho kimekuwa kilimwa na wakulima kutoka sehemu mbali mbali”, alisema.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.