Bungeni leo: Waziri Ummy awataka wanawake wa Kigoma kujiongeza

Alisema kuwa mkoa huo umepata magari sita kwa ajili ya huduma za afya na kumtaka Mbunge kuendelea kushirikiana na Wizara yake na ile ya Tamisemi katika...

Bungeni leo: Waziri Ummy awataka wanawake wa Kigoma kujiongeza

Alisema kuwa mkoa huo umepata magari sita kwa ajili ya huduma za afya na kumtaka Mbunge kuendelea kushirikiana na Wizara yake na ile ya Tamisemi katika...

05 June 2018 Tuesday 10:49
Bungeni leo: Waziri Ummy awataka wanawake wa Kigoma kujiongeza

Na Mwandishi wetu

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wanawake wa mkoa wa Kigoma kujiongeza ili kuboresha huduma za afya na mtoto ambazo ziko chini sana.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kasulu Daniel Nsanzugwanko (CCM) aliyetaka kujua sababu za mkoa wa Kigoma kutopewa kipaumbele katika huduma za afya.

Mbunge huyo alisema kuwa huduma za afya zipo chini sana kwani hospitali ya wilaya haina hata gari la kubebea wagonjwa.

Akjibu swali hilo, Waziri Ummy alisema kuwa si kweli mkoa huo haupewi kipaumbele kwa huduma za afya.Hata hivyo alikiri kuwa hali ya viashiria vya afya hasa ya mama na mtoto ni duni lakini serikali imekuja na mpango wa kuinua.

Alisema kuwa mkoa huo umepata magari sita kwa ajili ya huduma za afya na kumtaka Mbunge kuendelea kushirikiana na Wizara yake na ile ya Tamisemi katika kuboresha sekta hiyo.

Kuhusu huduma za afya kwa , alisema kuwa suala hilo ni la uelewa tu na kuhoji kivipi wanawake wa mkoa wa Kilimanjaro wanahudhuria kliniki lakini wa Kigoma wanashindwa.

Hata hivyo alidokeza kuwa katika kuinua huduma hiyo Wizara inatarajia kuzindua kampeni maalum ijulikanayo kama jiongeze jivute salama.

Aliongeza kuwa endapo wakina mama wa Mkoa huo wakijiongeza serikali haitosita kuendelea kuwahamisisha.

Waziri huyo alisema ili kuhakikisha akina mama wanahudhuria kliniki, serikali itaanza kutoa shilingi elfu 25 kwa kila zahanati ambapo mwanamke atakuwa amejifungulia.

Azania Post

Updated: 05.06.2018 12:42
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.