Waziri wa afya DRC ajiuzulu

Waziri wa afya DRC ajiuzulu

23 July 2019 Tuesday 12:38
Waziri wa afya DRC ajiuzulu

Kinshansa, DRC 
WAZIRI wa afya nchini  Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo(DRC) Oly Ilunga amejiuzulu wadhifa wake huo

Katika barua yake ya kujiuzulu, Oly Ilunga ameshutumu uamuzi wa rais Felix Tshisekedi kumteua mtu mwingine katika kikosi kinachokabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini humo.

Pia ameshutumu alichokitaja kuwa ni shinikizo la nje la kuidhinihsa chanjo za majaribio kwa ugonjwa huo. Mwaka uliopita mlipuko huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,700.
 
Wiki iliyopita shirika la afya duniani (WHO) lilitangaza kwamba mlipuko wa ugonjwa huo kuwa dharura ya afya ya kimataifa.

Janga la ugonjwa wa Ebola liliathiri sehemu kadhaa za Afrika magharibi kuanzia 2014 hadi 2016, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 11,000.

Katika barua yake kwa rais Felix Tshisekedi, ameshutumu uamuzi wa kumuondoa yeye kama kiongozi wa kikosi kinachokabiliana na Ebola na badala yake kuchaguliwa kamati iliyo "chini ya usimamizi wake binafsi".

Amesema wanakamati hao waliingia kazi yake katika miezi ya hivi karibuni.  Ameshutumu pia "shinikizo kubwa lililopo katika miezi ya hivi karibuni" kutumia chanjo ya majaribio ya Ebola inayopigiwa upatu na mashirika ya misaada na wafadhili.  Amesema chanjo iliyopo sasa ndiyo iliyothibitishwa kufanyakazi pekee.

Mlipuko wa hivi sasa - wa pili kwa ukubwa - ulianza mnamo Agosti mwaka jana na umeathiri  jimbo la Kivu  kaskazini na jimbo la Ituri.

Zaidi ya watu 2,500 wameathirika na ugonjwa huo huku thuluthi mbili ya idadi hiyo  ikifariki. Imechukua siku 224 kwa idadi ya visa kufika 1,000, lakini siku 71 za zaidi kwa idadi hiyo kufika 2,000.

Zaidi ya watu 2,000 wameripotiwa kuugua Ebola nchini DRC, visa 12 vipya vinaripotiwa kila siku. Asilimia 97 na zaidi ya watu 161,000 wamepewa chanjo hiyo kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

Mlipuko huo kwa sasa umetatizwa na mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya wahudumu wa afya na imani potofu kuhusu chanjo inayotolewa sasa.
Ebola ni nini?Ebola ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambapo aliyepata maambukizi hupata dalili za homa, uchovu, maumivu ya viungo na koo.
Kisha mgonjwa hutapika, kuharisha na kutoka damu.

Watu huambukizwa kwa njia ya kugusana, njia ya mdomo na pua, pia kwa njia ya damu, matapishi, kinyesi,majimaji ya kwenye mwili wa mtu mwenye Ebola

Wagonjwa hupoteza maisha kutokana na kupungukia maji mwilini na viungo kushindwa kufanya kazi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.