Ukibaka tu, nguvu za kiume zinaondolewa

Ukibaka tu, nguvu za kiume zinaondolewa

12 June 2019 Wednesday 08:16
Ukibaka tu, nguvu za kiume zinaondolewa

Alabama, Marekani

JIMBO  la Alabama nchini marekani limepitisha muswada wa sheria inayowalazimu baadhi ya watu waliopatikana na hatia ya kuwabaka watoto kupewa tiba ya kemikali itakayowaondolea uwezo wa nguvu za kiume.

Chini ya sheria hiyo, wale watakaopatikana na hatia ya kosa la kufanya tendo la ngono na watoto mwenye umri wa chini ya miaka 13 watalazimika kuanza kupata dawa za kuwapunguzia uwezo wa kufanya ngono mwezi mmoja kabla ya kuachiliwa kwa msamaha

Mahakama itaamua ni lini watakapokuwa hawahitaji tena dawa hiyo ya kikemikali.

Hadi sasa kuna majimbo saba , likiwemo Louisiana na Florida, yenye sheria ya kumaliza nguvu za kiume kwa wanaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto wadogo.

Muswada wa sheria hiyo ulitiwa saini na Gavana wa jimbo la Alabama Kay Ivey Jumatatu. "Hii ni hatua kuelekea kuwalinda watoto katika jimbo la Alabama," Alisema Bi Ivey.

Hatua hiyo awali ilipendekezwa na Mbunge wa chama cha Republican Steve Hurst. Alisema amekuwa akiathirika sana kwa kusikiliza ushahidi kutoka kwa mashirika yanayowalea watoto kuhusu namna watoto wadogo wanavyobakwa

Muswada huo umekosolewa na Muungano wa mashirika yanayopigania uhuru wa raia katika jimbo la Alabama. Mkurugenzi Mkuu wa Muungano huo Randall Marshall alikiambia kipindi cha told AL.com kuwa : "Haijawa wazi kwamba ni kweli zina athari yoyote na ikiwa imethibitishwa kimatibabu.

"Wakati jimbo linapoanzisha vipimo juu ya watu ,nadhani ni kinyume cha katiba ."

Kuondolewa uwezo wa kiume kwa njia ya kemikali ni nini?

Kwa matibabu ya kawaida mtu hupewa tembe au kwa njia ya sindano , ambavyo huzuwia uzalishwaji wa mbegu za uzazi za kiume na kuathiri uwezo wa mtu wa kuwa na hamu ya kufanya tendo la ngono.

Hata hivyo kwa kawaida mtu anaweza kurejeshewa uwezo huo wakati matibabu yanapositishwa.

Mwaka 2009, wafungwa kadhaa nchini Uingereza walishiriki katika mradi wa uchunguzi wa dawa hizo ambapo walipoteza uwezo wao wa kufanya ngono kwa njia ya kemikali.

Waliofanyiwa majaribio walikuwa ni wafungwa waliokuwa na "viwango vikubwa vya hamu ya ngono au matamanio makubwa ya kufanya tendo la ngono ".

Mwanasaikolojia wa Uhalifu Don Grubin alisema kuwa waliopewa dawa waliripoti kuwa na "mabadiliko katika maisha yao".

Mwaka 2016, Indonesia ilipitisha sheria inayoidhinisha matumizi ya kemikali katika kuzuwia nguvu za kiume kama hukumu ya chini na kunhgongwa kwa wanaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto. Wakati huo , Prijo Sidipratomo kutoka Shirika la madaktari wa Indonesia alitaja mbinu hiyo kuwa v yenye "madhara" na iliyo "kinyume na haki za binadamu".

Korea kusini ilipitisha sheria ya matumizi ya kemikali katika kuzuwia uwezo wa nguvu za kiume mwezi Julai, 2011.

BBC

Updated: 12.06.2019 08:43
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.