Afcon 2019 Wanyama aihofia Taifa Stars

Afcon 2019 Wanyama aihofia Taifa Stars

18 June 2019 Tuesday 09:21
Afcon 2019 Wanyama aihofia Taifa Stars

CAIRO, Misri
NAHODHA wa timu ya taifa ya Kenya 'Harembee' Victor Wanyama amesema  katika mashindano ya Afcon 2019 miongoni mwa timu anayoihofia ni timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Kiungo huyo ambaye ni mchezaji wa kimataifa, anayeichezea Tottenham  Spurs ya Uingereza amesema mechi ya Stars na Harambee itakuwa ni ya kufa na kupona.

"Timu ya Tanzania na Kenya zinaushindani wa asili, tukikutana ni kama 'Daby'. Ndio maana ninaihofia sana Stars. Naamini mechi yetu itakuwa ni ya kufa na kupona,'' amesema Wanyama alipokuwa akizungumza na BBC mapema leo.

Stars ipo kundi  C ikiwa na timu za Kenya, Senegal na Algeria. Inatarajiwa kukutana na Harembee katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo Julai mosi. Itafungua pazia kwa kucheza na Senegal Juni 23, 2019

Wanyama amesema pamoja na kwamba kundi lao ni gumu huku Harembee na Stars zikionekana kama 'underdog' lakini zitafanya maajabu yasiyotarajiwa.

Amesema kwa sasa soka la Afrika Mashariki linazidi kukuwa na ndio maana katika mashindano ya Afcon 2019 timu nne ikiwemo Uganda na Burundi zinashiriki.

Katika mechi za kujipima nguvu, Kenya iliifunga Ivory Coast goli 1-0 huku Stars ikisuluhu 1-1 na Zimbabwe na ikafungwa 1-0 na Misri.

Mashindano ya Afcon  2019  nchini Misri yanatarajia kuanza Juni 21, 2019

Updated: 18.06.2019 11:48
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.