Afcon 2019: Zidane aitabiria ubingwa Algeria

Afcon 2019: Zidane aitabiria ubingwa Algeria

25 June 2019 Tuesday 14:52
Afcon 2019: Zidane aitabiria ubingwa Algeria

Kocha wa Real Madrid ya Hispania, Zinedine Zidane anaamini timu ya taifa ya Algeria inaweza kutwaa ubingwa wa fainali za mataifa ‘AFCON’ zinazofanyika kwa mara ya tano nchini Misri.

Algeria wameanza vizuri fainali za AFCON kwa kuifunga Kenya kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kwa mabao 2-0, Jumapili iliyopita jijini Cairo.

Zidane ambaye ni Mfaransa mwenye asilia ya Algeria, alisema  hayo alipokuwa akizungumza na chombo cha luninga cha beIN SPORT na kwamba hiyo ni kutokana na kiwango walichokionyesha Algeria  katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Kenya.

"Tunataka kuona timu ya taifa ya Algeria ikicheza vizuri kwaajili ya watu wa Algeria,” alisema Zidane ambaye anashikilia rekodi ya kuiongoza Real Madrid kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu mfululizo.

Algeria, ambao wametwaa ubingwa wa AFCON mara moja ndani ya mwaka 1990, wapo kundi C na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’,  Senegal na Kenya.

"Nahitaji kuona wakishinda ubingwa ili kuona shangwe itakavyotawala  kwenye mitaa,” aliongeza kiungo huyo wa zamani wa Juventus na Real Madrid.

Updated: 26.06.2019 09:22
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.